• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
KAFYU: Mwanabodaboda afariki baada ya kugongana na lori akiogopa polisi

KAFYU: Mwanabodaboda afariki baada ya kugongana na lori akiogopa polisi

Na Waweru Wairimu

Mwendeshaji wa bodaboda alikufa baada ya pikipiki yake kugongana na lori eneo la Maili Saba, Kaunti ya Meru akitoroka maafisa wa polisi waliokuwa wakitekeleza amri ya kutotoka nje usiku.

Na ingawa polisi wanadai kuwa kisa hicho kilitokea saa moja jioni, mwanabodaboda aliyekuwa nyuma ya marehemu wakielekea Isiolo aliambia Taifa Leo kwamba mwanamume huyo aliyetambuliwa kwa jina Kithinji aligongwa saa mbili na nusu usiku Kulingana na mwanabodaboda huyo ambaye alifaulu kutoroka, marehemu aligongana na lori alipokuwa akihepa gari la polisi lililokuwa limeegeshwa katikati ya barabara muda mfupi baada ya kushusha abiria.

“Gari hilo la polisi lilikuwa likitufukuza na marehemu alipokuwa akishusha abiria, lilimzuia kutoka mbele,” alieleza bodaboda aliyetoroka kuepuka ghadhabu za polisi.

Wakazi waliofika eneo hilo kutoka makwao walizuiwa kukaribia mwili. Mkuu wa polisi katika kaunti ndogo ya Buuri Joseph Asugo alithibitisha kisa hicho lakini akasema bodaboda huyo aligongwa na lori alipokuwa akiingia kwenye barabara kuu.

“Aligongwa akiingia barabara kuu kutoka barabara nyingine na akafariki papo hapo,” alisema Bw Asugo akiongea na Taifa Leo kwa simu

You can share this post!

Waumini wa Kavonokya wasema wanaogopa polisi kuliko corona

Wang’atwa na nyuki wakila uroda

adminleo