CORONA: Waziri wa Fedha Ujerumani ajiua
MASHIRIKA NA FAUSTINE NGILA
WAZIRI wa mmoja nchini Ujerumani amejiua baada ya kuelezea kulemewa kupata mikakakati ya kufufua uchumi wa taifa hilo ambao umezama kutokana na gonjwa la cocorna, afisa mkuu wa serikali aliambia mashirika ya habari.
Bw Thomas Schaefer, ambaye alikuwa waziri wa fedha katika eneo la Hesse, alipatikana amefariki baada ya kujiua hapo Jumamosi katika reli ya Hochheim, iliyo karibu na mji wa Frankfurt.
Gavana wa eneo hilo Volker Bouffier alisema waziri huyo wa miaka 54 alikuwa na msongo wa mawazo kuhusu jinsi ya kushughulikia hali ya uchumi katika nyakati hizi za ugonjwa wa corona ambao umeangusha masoko yote duniani.
Aisema Schaefer alikuwa anajishughulisha sana na kufikiria “iwapo itawezekana kutimiza matakwa ya mamilioni ya wakazi, hasa kuhusu msaada wa kifedha.”
“Ninaamini dhiki na hofu hii ilikuwa nzito kwake. Yamkini hangeweza kupata suluhu. Alikuwa amekosa matumaini na akatuacha,” Bouffier alisema.
Maafisa wanaochunguza kifo hicho walisema walithitibitisha kuwa Schaefer alijitia kitanzi baada ya kuwapeleleza waliokuwa karibu naye.
Schaefer alikuwa mwanachana wa chama cha Chansela Angela Merkel cha Christian Democratic Union na alikuwa ameshikilia wadhifa huo kwa miaka kumi.