Maseneta wenye zaidi ya miaka 58 kufanyia kazi nyumbani
NA DAVID MWERE
Spika wa Seneti Ken Lusaka ametangaza hatua zitakazoruhusu maseneta 28 pekee kuendelea kuhudhuria vikao vya seneti.
Hii, alisema, ni mojawapo ya mbinu za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.
Maseneta na wafanyakazi wa seneti walio na zaidi ya miaka 58 wameakiwa kufanyia kazi nyumbani kufuatia agizo la Rais Uhuru Kenyatta.
“Ninawarai maseneta wote na wafanyakazi wa afisi za seneti kufuata mwongozo huu ili kutoa fursa kwa mijadala kuendelea huku tukijikinga. Nitatoa maelezo zaidi ikibidi,” Bw Lusaka akasema.
Orodha ya maseneta 28 ilifikiwa wakati wa kutano wa mpingao ya mijadala ya seneti hapo Jumatatu.
IMETAFSIRIWA NA FAUSTINE NGILA