• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 6:47 AM
CORONA: Kenya yasubiri Sh5 bilioni kutoka Benki ya Dunia

CORONA: Kenya yasubiri Sh5 bilioni kutoka Benki ya Dunia

NA JOHN MUTUA

Kenya inatarajia kupokea msaada wa Sh5.2 bilioni kutoka kwa Benki ya Dunia utakaosaidia kupambana na ugonjwa wa corona.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema kuwa pesa hizo zitasaidia pakubwa katika kufadhili utengenezaji wa barakoa, dawa ya kunawa mikono, mavazi ya maafisa wa afya ya kujikinga dhidi ya mmambukizi ya corona na kuongezaea vitanda vya wagongjwa wa corona.

Ufadhili huo unakuja huku Kenya ikithibitisha visa vingine 22 vipya Jumatano huku hofu ya idadi hiyo kuongezeka siku za usoni ikiwa juu.

Waziri Kagwe alionya kuwa kuna uwezekano wa kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa corona siku zijazo iwapo Wakenya hawatafuata maagizo ya serikali ya kutotangamana na kuzingatia usafi kwa kuosha mikono kwa kutumia maji na sabuni

Bw Kagwe alisema kuwa Kenya itaongezea utengenezaji wa barakoa na pia usambasaji wa viyeyushi.

Benki ya Dunia wiki iliyopita ilitoa msaada wa mashine 250 za kupumua huku bilionea wa China na mwazilishi wa kampuni ya mauzo ya mitandaoni Alibaba Jack Ma alitoa msaada wa vifaa 25,000 vya kupima corona.

Tafsiri na FAUSTINE NGILA

You can share this post!

CORONA: Wauzaji nguo walia hela hazipatikani

CORONA: Ukaidi wa Wakenya unavyolemaza juhudi za kupunguza...

adminleo