Polisi wakabili wezi wa mabati na vyuma vya mamilioni
NA RICHARD MAOSI
Wakazi wa Nakuru siku ya Jumanne walihatarisha maisha yao, kwa kuiba mali ya mamilioni ya pesa kutoka kwenye kiwanda, kilichokuwa kimebomolewa na usimamizi wa baraza la kaunti.
Baadhi yao wakiwa ni mafundi kutoka sekta ya Jua Kali walinaswa na kamera wakiwa wamebeba mabati, mitungi na vyuma kutoka kwenye kampuni hiyo inayofahamika kama Mombasa Maize Millers.
Bila kupisha magari yaliyokuwa yakipita barabarani kwa kasi, waliendelea shughuli kama kawaida
Wachache waliokubali kuzungumza na Taifa Leo Dijitali wanasema ni kama Krismasi ilikuwa imekuja mapema kwao mwaka huu 2020, licha ya hali ngumu ya maisha kuwakabili.
Tangu mkurupuko wa Covid 19 kutangazwa, wengi wao walikuwa wamepoteza nafasi za ajira, na kubakia majumbani pao.
“Nilikuwa nikitembea nilipowaona vijana wakinyakulia chuma na mimi nikaamua kuchukua mabati,ili nikauze kwa fundi wa kutengeneza jiko mtaani Bondeni,”akasema mmoja wao ambaye alitaka tubane jina lake.
Bila kujali hatari ya kuambuzikana maradhi ya Covid -19, vijana hao walikaribiana na hata kuvuta vyuma kwa pamoja wakishirikiana..
Ilibidi polisi kutumia vitoa machozi, ndipo kila mmoja akatorokea usalama wake huku sehemu yenyewe ikibakia chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Duru za kuaminika zinasema sehemu hii ilikuwa imetengewa kutengeneza sjeji ya kuegesha magari ya uchukuzi. lakini wenyeji walikuwa wamekaidi amri ya kuondoka.
Hili linajiri siku chache baada ya steji ya magari kuondolewa katikati ya mji wa Nakuru. katika hatua ya kupunguza msongamano wa magari na watu wakati serikali ikipambana na Covid-19′
Wakati wa mkasa huo hakuna aliyejuruhiwa.