• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
RAHAB MWENDE: Ninafuata nyayo za Ruth Wamuyu katika usanii wa injili

RAHAB MWENDE: Ninafuata nyayo za Ruth Wamuyu katika usanii wa injili

Na JOHN KIMWERE

ALIANZA kujituma katika masuala ya muziki wa injili akiwa na umri wa miaka 13 ambapo analenga kujituma kiume kuhakikisha unapata mpenyo na kutambulika kote duniani.

Kando na uimbaji, Rahab Mwende Gathuru anaodhoreshwa kati ya waigizaji chipukizi wa kike wanaoibukia hapa nchini ingawa hakuna filamu aliyowahi kushiriki na kupata nafasi kuonyeshwa kwenye runinga.

”Ninaamini nina talanta katika utunzi wa nyimbo za injili bila kuweka katika kaburi la sahau uigizaji ambapo nimekuwa nikishiriki shoo mbali mbali kwenye kumbi za burudani,” anasema na kuongeza kuwa anaaminia Mungu atamfungulia milango miaka ijayo.

Anasema kuwa alipata mwito wa kughani nyimbo za injili akiwa mwanafuzi wa darasa la sita maana alilelewa maisha ya Kikanisa. Kipusa huyu mwenye umri wa miaka 23 anasema katika uimbaji wa injili analenga kumpiku mwimbaji na muhubiri, Ruth Wamuyu.

Msanii huyu anajivunia kutunga nyimbo nyingi tu katika uimbaji wake ikiwemo: ‘Ngai Murathimi (Mungu mwenye kubariki),’ ‘Naijulikane’, ‘Wi Muthaka(Yu mwema)’ ‘Amukira Ngatho(Pokea sifa),’ na Ni Gukena(Ni kufurahi)’ kati ya zinginezo.

Katika mpango mzima msichana huyu amefanikiwa kutunga nyimbo sita za audio tangia aanze kujituma katika masuala ya muziki mwaka 2018. Demu huyu ameghani nyimbo kama: ‘Korwo ni Mundu(Kama ni mtu),’ ‘Wendo wa Mutharaba (Upendo wa Msalamba),’ ‘Hee hinya (Nipe Nguvu),’ ‘Mihaka (Mipaka),’ ‘Uthingu (Mtakatifu)’ na ‘Kihoti (Muweza).’ Mwimbaji huyu anasema analenga kutoa video ya nyimbo hizo kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Katika masuala ya uigizaji anasema anatamani zaidi kushiriki filamu na kuonyeshwa kwenye runinga ili kumfungulia milango katika tansia hiyo. Kadhalika anasema uigizaji ni ajira kama zingine.

Kwa waigizaji wa humu wa nchini anatamani kufikia kiwango cha Celestine Gachuhi maarufu kama Selina. Katika kiwango cha kimataifa anapania kutinga hadhi ya mwigizaji wa filamu za Kinigeria(Nollywood), Jackie Appian.

Msanii huyu anajivunia kuigiza filamu nyingi tu kama ‘Divine Love,’ ‘Princess Tyra,’ ‘The Perfect Picture,’ ‘Mummys Daughter,’ ‘The king is Mine na ‘Heart of men’ kati ya zingine.

USHAURI

Msichana huyu sio mchoyo wa mawaidha anatoa mwito kwa wenzake wawe wakitunga nyimbo zilizo na maudhuhi ya kulea Wakristo kiroho.

Pia anawaambia waelewe kuwa utunzi ni mwito na wanastahili kuisha maisha ya Kikristo ili kuwa mfano mwema kwa wafuasi wao na jamii kwa jumla.

Anashauri chipukizi wenzake kukaza buti katika kazi zao na wavumilie changamoto zote wanazopitia katika sekta ya burudani ya muziki na maigizo.

Anadokeza kuwa vyombo vya habari humu nchini vinastahili kuanzisha vipindi nyingi kucheza muziki na kuonyesha filamu za wazalendo.

Anasema anakumbuka wakati mamake alichoma kitabu chake alichochokuwa ameandika zaidi ya nyimbo 20.

”Kusema kweli utunzi sio rahisi kwa kuzingatia suala la ufadhili limeibuka donda sugu,” akasema na kuongeza kuwa kwa upande wake hayupo katika usanii kwa sababu ya pesa mbali analenga kutunga nyimbo za kujenga Wakristo kiroho.

Kadhalika anasema hujipata katika hali tete kwa kupondwa na wafuasi wao wasifurahishwa na tambo zao.

You can share this post!

MR BEE: Mmliki wa studio ya kunoa vipaji vya chipukizi

Wakazi walia nzige wamekula mimea inayoota msimu wa upanzi

adminleo