• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:25 PM
NASAHA: Wanawake waliopewa udhuru Ramadhan na wanachotakiwa kufanya

NASAHA: Wanawake waliopewa udhuru Ramadhan na wanachotakiwa kufanya

Na MISHI GONGO

RAMADHAN ni Mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu.

Funga au Saumu katika mwezi huo ni nguzo ya nne katika dini hiyo, na inamlazimu kila Mwislamu aliyebalehe na mwenye afya nzuri kufunga.

Waumini wa dini ya Kiislamu huamini kuwa mwezi huo ni wa kujisafisha na kujiweka karibu na Muumba.

Watu huongeza ibada za swala na kutoka sadaka kama njia ya kupata neema za Mwenyezi Mungu.

Hata hivyo, kuna baadhi ya watu waliokatazwa kushiriki katika ibada hiyo muhimu.

Miongoni mwao ni wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha watoto.

Mwenyezi Mungu ameamrisha wanawake walio katika hali hizo na wanahofia kupata matatizo ya kiafya kutokana na saumu kutofunga. Hata hivyo, wanalazimika kulipiza siku walizoacha.

Wengine waliopewa udhuru wa kutekeleza ibada hiyo ni wanawake walio katika hedhi au wanaopata damu ya uzazi.

Japo watu hao wamekatazwa kushiriki katika kufunga Ramadhani, yapo matendo ambayo wanaweza kuyafanya ili kupokea baraka na neema za Mwenyezi Mungu kama wengine waliofunga.

Miongoni mwa matendo wanayoweza kushiriki ni kutoa sadaka, kusikiliza Qur’an, kuwalisha wasiojiweza katika jamii, kusikiliza mawaidha kutoka kwa mwalimu wa dini na kadhalika.

Nguzo za Uislamu ni tano; nazo ni: Shahada, Swala tano kwa siku, kutoa Zaka, Saumu, na hatimaye Kuhiji Mecca.

You can share this post!

Matumaini huku waliopona corona wakifika 124

MKASA: Stovu yasababishia familia majeraha

adminleo