• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 2:10 PM
Wanaoshtakiwa kumuua mwanahabari kusalia ndani

Wanaoshtakiwa kumuua mwanahabari kusalia ndani

Na RICHARD MUNGUTI

Washukiwa wanne wanaodaiwa walimuua mtangazaji wa kituo cha Redio cha Pamoja FM kilichoko mtaa wa mabanda wa Kibra wataendelea kuzuiliwa korokoroni kwa siku saba zaidi.

“Afisa wa polisi anayechunguza kesi hii hajakamilisha mahojiano na washukiwa hawa wanne.Anahitaji siku nyingine saba,” kiongozi wa mashtaka James Gachoka alimweleza hakimu mwandamizi Kennedy Cheruiyot Jumanne.

Gachoka alisema kuna washukiwa wengine wawili wanaoendelea kusakwa na polisi waliotajwa na washukiwa wanaoemdelea kuhojiwa.

Hakimu alifahamishwa jamii wanamoishi washukiwa ilighadhanishwa na mauaji ya Mohammed Hassan Marjani mnamo Mei 4.

“Ijapokuwa dhamana ni haki ya washukiwa itabidi wazuiliwe kwa siku nyingine saba ili uchunguzi ukamilishwe,” Gachoka alimweleza hakimu.

Mahakama iliombwa imruhusu afisa anayechunhguza kesi hii Pascal Mwachiro akamilishe uchunguzi.

Waliokamatwa kufuatia mauaji ya Marjani ni Juma Hussein Mohammed, Shahidi Jabir, Juma Hussein na Luqman Mohammed.

Wanne hao waliagizwa wazuiliwe kwa siku nne zaidi katika kituo cha polisi cha Kilimani.

Wote wanahojiwa kiuhusu mauaji ya Marjani aliyeuawa akitoka kazini asubuhi ya Mei 4 2020 katika mtaa Lindi Kibra.

“Naomba hii mahakama iamuru mshukiwa azuiliwe kuhojiwa na kupelekwa kupimwa akili ibainike ikiwa ni timamu,” afisa anayechunguza mauaji hayo aliambia Ochoi.

Juma alishikwa katika bustani ya Uhuru Park akijaribu kutoroka.

Juma atashtakiwa pamoja na MarjaniLuqman Mohammed Ibrahim aliyeshikwa wiki iliyopita na kufikishwa kortini.

Akiwasilisha onbi la kuzuiliwa kwa Luqman afisa wa polisi Paul Mwachiro alimweleza hakimu mkazi Carolyne Muthoni Nzibe kuwa mshukiwa alitiwa nguvuni Jumatatu na mahojiano yanaendelea.

Mwachiro alisema mshukiwa huyu anatazamiwa kuwasaidia polisi kuwasaka washukiwa wengine alioshirikiana nao kutekeleza uhalifu huo wakiwa wamejihami na silaha hatari.

Hakimu alifahamishwa mshukiwa anahitajika kupimwa akili ibainike ikiwa akili yake ni timamu kabla ya kufunguliwa mashtaka.

Bi Nzibo aliombwa aamuru mshukiwa azuiliwe siku 14.

Mahakama iliambiwa Marjan mwenye wa miaka 62 alishambuliwa na kundi la wanaume saba waliokutana naye katika eneo la Olimpiks akitoka kazini na kumshambulia.

Aliaga dunia baada ya muda mfupi.

You can share this post!

SANAA: Mwanamuziki wa Injili anayetangaza huduma maarufu ya...

TAHARIRI: Ukaidi wa Tanzania tishio kwa eneo zima

adminleo