• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Viongozi wa jamii ya Kindiki waikemea Jubilee kumvua mamlaka

Viongozi wa jamii ya Kindiki waikemea Jubilee kumvua mamlaka

NA DAVID MUCHUI

Viongozi wa kisiasa kutoka kaunti za Mlima Kenya mashariki wamekemea uamuzi wa seneti kumung’oa Seneta Kithure Kindiki kutoka kwa wadhifa wa Naibu Spika wa seneti.

Wabunge kutoka Meru, Embu na Tharaka Nithi walilaumu uongozi wa chama cha Jubilee kwa kutenga viongozi kutoka mashariki ya Mlima Kenya.

Bw Josphat Gichunge wa Tingania Mashariki, John Mutunga wa Tingania Magharibiki, Mugambi Rindikiri wa Buuri, Moses Kirima wa Imenti ya Kati, Gitonga Murugara wa Tharaka, Patrick Munene wa Chuka Igamba Ngombe, Mwakilishi Mwanamke wa Tharaka Nithi Bi Beatrice Nkatha na seneta Linturi wamesema wametamaushwa na hatua hiyo.

Bw Linturi alisema kuwa ilikuwa wazi kuanzia mwanzo kuwa chama hicho kilikuwa tayari kumtia adabu Prof Kindiki.

“Tulijua hatungemwokoa, lakini singeunga mkono kumtoa mamlakani. Singepiga kura ya kumng’atua kwa sababu hajafanya lolote baya,” Bw Linturi alisema.

Tafsiri: Faustine Ngila

You can share this post!

Sofapaka wataka AFC Leopards waombe msamaha kwa kuwadunisha

Staa wa Shujaa Allan Makaka afariki

adminleo