• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
KRA yapungukiwa na Sh17 bilioni

KRA yapungukiwa na Sh17 bilioni

Na BERNARDINE MUTANU

Shirika la Kutoza Ushuru nchini (KRA) lilikosa kupata zaidi ya Sh17 bilioni kama ushuru.

Hii ni baada ya serikali kuondolea ushuru vifaa na nyenzo za utengezaji wa reli ya kisasa (SGR) vilivyoagizwa nchini, vifaa vya jeshi na polisi.

Shirika hilo lilikosa mapato ya Sh17.9 bilioni kutokana na ushuru huo na bidhaa zingine kuhusiana na uagizaji.

Ripoti hii inatokana na takwimu za faragha kutoka kwa KRA, lakini zilizopatikana na wanahabari.

Habari hiyo ya KRA inaonyesha kuwa upungufu huo pia ulitokana na kutolewa ushuru kwa chakula kilichoagizwa nchini na wafadhili kwa lengo la kuwasaidia wananchi waliokuwa wakiathiriwa na njaa.

SGR lilikua shirika lililonufaika zaidi kutokana na kuondolewa kwa ushuru. Ujenzi wa reli hiyo unafadhiliwa na Serikali ya China kwa thamani ya Sh447 bilioni ikiwemo ni pamoja na gharama ya ufadhili.

Bidhaa zilizoagizwa nchini kwa ujenzi wa SGR kati ya Machi na Julai 2017 ziliondolewa ushuru wa Sh5 bilioni.

Bidhaa za KDF kati ya Machi na Julai 2017 ziliinyima KRA Sh1.96 bilioni ilhali mahindi, sukari na maziwa yaliinyima KRA 276 milioni.

Pia, vifaa na bidhaa zilizoagizwa na polisi ziliinyima KRA Sh1.2 bilioni.

You can share this post!

SportPesa kufadhili FKF, KPL, Gor na Ingwe

Mvua inayonyesha kuchangia kushuka kwa ada ya umeme

adminleo