• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 5:23 PM
Miradi ya Ajenda Nne Kuu kuongeza mikopo kutoka Uchina

Miradi ya Ajenda Nne Kuu kuongeza mikopo kutoka Uchina

Na BERNARDINE MUTANU

Huenda azma ya serikali kutekeleza ajenda ya maendeleo ikaongeza mikopo kutoka China kufikia 2022 kuwa Sh1 trilioni.

Hii ni baada ya China kuahidi kufadhili ajenda ya maendeleo ya serikali katika muda wa miaka mitano ijayo.

Kwa sasa, China inaongoza mataifa wafadhili wakuu wa miradi ya maendeleo Kenya ambapo kufikia sasa serikali hiyo imefadhili miradi kwa gharama ya Sh730 bilioni ambapo mikopo ni Sh702.1 bilioni na msaada wa Sh27.9 bilioni.

Kulingana na Katibu Mkuu katika Wizara ya Fedha Kamau Thugge, “Big Four Agenda” itagharimu pesa nyingi na alikuwa akitarajia kuwa serikali itashirikiana na mashirika ya kibinafsi ili kutekeleza mpango huo.

Alisema serikali inatumia mkopo kutoka China kujenga sehemu ya reli ya kisasa(SGR) kati ya Nairobi na Naivasha, ujenzi wa depo ya Nairobi, Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kenyatta na ujenzi wa Barabara ya Kibwezi kuelekea Kitui miongoni mwa miradi mingine.

Katibu huyo aliongeza kuwa kulikuwa na miradi zaidi inayohitajika kutekelezwa.

You can share this post!

Carrefour yabisha Westlands

Serikali kununua treni 18 za abiria kufikia 2019

adminleo