Baa la njaa laja corona ikienea – WHO
By BERNADINE MUTANU
Huku Kenya ikiendeleza vita dhidi ya virusi vya corona, Wakenya wengi wameanza kukumbwa na baa la njaa huku watoto wakiathiriwa zaidi.
Shirika la Afya Duniani {WHO} imeonya kwamba hali hii inaweza kuzua utapiamlo kwa kiasi kikubwa barani Afrika.
“Athari ya janga hili la corona inatarajiwa kuwalemea wanaokumbana na upungufu wa chakula, wakati utoshelevu wa chakula uko mashakani kwa sababu ya vikwazo vilivyowekwa vya kusafirisha chakula”, Mkurungezi Matshidiso alisema.
Tayari Kenya imekuwa na changamoto mbalimbali katika kuhakikishia wananchi chakula cha kutosha. Katika uchunguzi uliofanywa hivi majuzi, Kenya ilpata alama ya 25.2 katika utoshelevu wa chakula huku ikisalia nambari 86 kati ya nchi 117 zilizofanyiwa utafiti.
Kutokana na vikwazo vilivyowekwa, familia nyingi haziwezi kumudu kupata chakula bora, huku maisha ya watoto yakiwa matatani.