• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 5:55 AM
Zoom inavyotumika Meru kuwafaa wasiojiweza

Zoom inavyotumika Meru kuwafaa wasiojiweza

Na CHARLES WANYORO

Wanachama wa kundi la vijijini eneo la Uruku katika Kaunti ya Meru wanatumia mikutano ya mitandaoni kuhamasishana kuchanga fedha kusaidia wenzao walioathirika vibaya na janga la corona.

Kupitia mikutano hiyo ya programu za simu ya Zoom wameweza kuwachangia pesa wazee, walemavu na wasiojiweza katika vijiji vinne huku pia wakiwapa watu 130 barakoa, viyeyuzi na chakula tangu mwezi Aprili..

Kupitia muungano huo, wanachama hutoa pesa, mazao na vyakula vinginevyo vinavyopewa wasiojiweza katika jamii.

Katibu wa kikundi hicho Paul Mwenda alisema kwamba walibuni wazo hilo baada ya kugundua kwamba kuna wanajamii walioathirika sana na kukosa chakula baada ya janga la corona kusababisha biashara kufungwa kwenye mji wa Nkubu.

Wamekuwa wakiandaa mikutano kupitia mitandao mara kwa mara wakiwashikisha wakazi wanaoishi katika miji mingine ili kusaidia wenzao nyumbani.

Chifu wa Uruku Dorothy Kinyua alisema kwamba mazao ya shambani yamekuwa yakiuzwa kwa mahoteli awali lakini sasa hayana faida kwa kukosa wanunuzi.

Alisema kwamba kuna watoto walemavu wengi waliokuwa wakifaidika na chakula cha shule lakini sasa wanashughulikiwa kutoka nyumbani.

You can share this post!

Nzige watisha kuzua baa la njaa Turkana

Waiguru akataa kuidhinisha fedha za ziada kwa bajeti ya...

adminleo