• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
COVID-19: Visa jumla ni 2,862 ambapo waliopona ni 849 huku idadi ya waliofariki ikifika 85

COVID-19: Visa jumla ni 2,862 ambapo waliopona ni 849 huku idadi ya waliofariki ikifika 85

Na CHARLES WASONGA

KULINGANA na takwimu zilizosomwa Jumatatu na Waziri Msaidizi wa Afya Rashid Aman idadi ya maambukizi mapya imekuwa visa 95 huku wagonjwa waliopona na kuruhusiwa kwenda nyumbani wakiwa 97 katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Sasa visa jumla kuwahi kuthibitishwa nchini ni 2,862

Kwa hivyo kufikia Jumatatu idadi ya jumla ya waliopona na 849.

Visa hivyo vipya 95 vilithibitishwa baada ya sampuli 1,096 kufanyiwa uchunguzi ndani ya kipindi cha saa 24.

Kufikia sasa jumla ya sampuli 98,439 zimepimwa tangu kisa cha kwanza cha Covid-19 kugunduliwa nchini Kenya..

Kati ya wagonjwa 95 wapya; 92 ni Wakenya huku watu wakiwa raia wa mataifa ya kigeni.

Kulingana na takwimu za Jumatano, Mombasa inaongoza kwa kuandikisha visa 56, Nairobi (13), Busia (10), Kajiado (6), Kilifi (3) huku Kitui, Kwale na Marsabiti zikiandikisha kisa kimoja kila moja.

Kaunti ya Marsabit ndiyo ya hivi punde kujiunga kwenye orodha ya kaunti ambazo zimeandikisha visa vya maambukizi ya Covid-19, ambazo sasa ni 38

Katika kaunti ya Nairobi, eneo bunge la Kibra bado linaongoza kwa kuandikisha maambukizki 10 huku maeneo ya Kasarani, Dagoreti Kaskazini na Kasarani zikiandikisha kisa kimoja kila moja.

Nalo eneobunge la Mvita linaongoza kwa idadi ya maambukizi mapya katika Kaunti ya Mombasa likifuatwa na Changamwe yenye visa 13, Nyali (7), Kisauni (6), Likoni (5) na Jomvu (3).

Na mgonjwa mmoja alifariki na hivyo kupandisha idadi ya maafa kutokana Covid-19 kuwa 85 kufikia Jumatatu.

Wakati huo huo wahudumu wa afya wawili katika Kaunti ya Nyeri wameambukizwa virusi vya corona.

Dkt Aman amesema wizara inafanya kila iwezalo ili kusambaza vifaa vya kujikinga kwa wahudumu wa afya kote nchini.

“Wahudumu wa afya wanakabiliwa na hatari kubwa kwa sababu wao ndio hushughulika na wagonjwa wa Covid-19 moja kwa moja kila siku. Kwa hivyo, tunasambaza vifaa vya kujikinga, sanitaiza na kuhakikisha kuwa wanafanya kazi katika maeneo ambapo wanaweza kujitenga kwa umbali wa mita moja na nusu,” akasema Dkt Aman.

You can share this post!

Diwani motoni kuhusu kifo cha mkewe

Madiwani wa Jubilee waitwa na Tuju ofisini

adminleo