• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Waiguru atia bidii juhudi za kuzima kutimuliwa

Waiguru atia bidii juhudi za kuzima kutimuliwa

Na WAANDISHI WETU

GAVANA wa Kirinyaga Anne Waiguru amefika mahakamani kwa mara ya pili kujaribu kuzima hatua ya kumng’oa mamlakani.

Bi Waiguru alitaja hatua hiyo kuwa kinyume cha sheria, kwa kuwa Mahakama Kuu ilikuwa imesimamisha utaratibu wa kumtimua mamlakani kwa sababu ya janga la corona.

Bi Waiguru alifika mahakamani kujaribu kuzuia utaratibu huo, huku Seneti ikipokea barua ya uamuzi wa madiwani kumuondoa mamlakani.

Kwenye barua kwa Spika wa Seneti, Ken Lusaka, Spika wa bunge la Kaunti ya Kirinyaga, Anthony Gathumbi alisema madiwani walifuata sheria kumtimua Bi Waiguru.

“Kwenye kikao leo asubuhi Juni 9, 2020, kupitia mswada ulioungwa mkono na madiwani 23 ikiwa ni zaidi ya thuluthi mbili, bunge lilipitisha hoja ya kumuondoa ofisini Gavana Anne Waiguru,” Bw Gathumbi alisema kwenye barua yake Jumanne.

Barua hiyo ilimfikia Bw Lusaka jana Jumatano na sasa anatarajiwa kuandaa kikao cha Seneti kujadili hatua ya madiwani wa Kirinyaga ikiwa ni pamoja na kumwita Bi Waiguru kujitetea.

Bw Lusaka alisema ameita mkutano wa kamati ya shughuli za Seneti kuamua suala hilo litakavyoshughulikiwa.

Kamati hiyo inaweza kuamua kuunda kamati ya maseneta 11 kushughulikia suala hilo au kuamua lishughulikiwe kwenye kikao cha maseneta wote ilivyofanyika wakati madiwani wa Kiambu walipomtimua Ferdinand Waititu.

TF Body text: Bi Waiguru anakabiliwa na madai ya kukosa kukosa kutoa hotuba ya kila mwaka kuhusu hali ya kaunti, kukiuka sheria za ununuzi, kutumia Sh10 milioni akidai ni za safari ingawa hakusafiri na kuwanyima wakazi wa Kirinyaga haki zao za huduma za afya.

TF Body text: Wakati huo huo, vita vya maneno viliibuka kuhusiana na kung’olewa kwa Bi Waiguru.

TF Body text: Waziri wa Utumishi wa Umma na Jinsia, Prof Margaret Kobia, katika taarifa yake alionekana kumuunga mkono Bi Waiguru ameonewa kwa kuwa ni mwanawake mwenye ujasiri.

Hata hivyo, taarifa yake ilichemsha mitandao ya kijamii ambapo alishtumiwa vikali, huku baadhi wakitaka kujua hakuteta wakati aliyekuwa kiranja wa wengi katika Seneti Susan Kihika na mwenzake wa Bunge la Kitaifa Cecily Mbarire walipovuliwa madaraka.

“Kwa Kobia baadhi ya wanawake ni sawa kuliko wenzao. Huenda Waiguru ni ‘zaidi ya mwanamke’ kushinda Cecily Mbarire na Susan Kihika!” Mbunge wa Mathira, Rigathi Gachagua alisema.

 

Ripoti ya MAUREEN KAKAH, BENSON MATHEKA na LUCY KILALO

You can share this post!

Samboja apokea mashine za kupambana na Covid-19

Wandani wa Ruto eneo la Rift Valley sasa wafyata ndimi

adminleo