Apigwa mawe hadi kifo kwa kuiba mahindi

NA ALEX NJERU

Wakazi waliokuwa na ghadhabu walimvamia na kumuua mwanamume wa miaka 30 kwa kusemekana kuiba mahindi mabichi katika shamba la jirani, kaunti ya Tharaka Nithi.

Chifu wa Ntoroni Paul Kiricho Mati alisema kwamba mwanamume huyo alipigwa mawe hadi kifo na mwili wake kuchomwa. Chifu huyo alisema kwamba akipokea habari hizo mshukiwa huyo tayari alikuwa ameteketezwa.

“Mwenye shamba hilo alipiga ukemi alipopata mwendazake akiiba mahindi shambani mwake. Majirani waliitikia kwa haraka wakamshika mshukiwa na wakaampiga mawe na baadaye wakachoma mwili wake,” alisema Bw Mati.

Maafisa wa polisi wa Makutano walichukua mwili huo wakaupeleka kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Chuka.

Jamaa wa mshukiwa wamekataa kwamba mwanawao aliuawa akiiba mahindi na wakaomba polisi kufanya uchunguzi.

Habari zinazohusiana na hii