Habari Mseto

Rais mpya wa Burundi aapishwa

June 18th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA AFP

Rais mpya wa nchi ya Burundi Jenerali Evariste Ndayishimiye ameapishwa Alhamisi kufuatia kifo cha rais aliyemtangulia Pierre Nkurunziza aliyemwachia nchi iliyojaa masaibu ya kisiasa na kiuchumi.

Ndayishimiye alichanguliwa Mei na alikuwa achukue afisi mwezi wa nane.

Kutambulishwa kwake kuliharakishwa baada ya kifo cha rais aliyemtangulia Nkurunziza kufariki.

Kuapishwa kwake kumefanyika katika uwanja wa michezo wa Ingoma katika mji wa Gitenga ,huku wananchi wakiombwa kufika mapema ili watekeleze matakwa ya kudhibiti corona ya kuosha mikono na kuangaliwa joto.

Wanadiplomasia na wawakilishi wa shirika za kimataifa walialikwa, hata hivyo ni rais wa Demokrasia ya Congo aliyealikwa pekee kuhusiana na janga la corona.

Nkurunziza aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 15 alisemekana kufariki kutokana na mshtuko wa moyo wiki iliyopita.

Hata hivyo Rais huyo wa mika 55 aligonjeka wiki mbili kabla ya mke wake kuletwa Nairobi kwa matibabu ya corona kulingana na taarifa ya matibabu.