• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Viongozi wa kidini wataka fursa ya kutakasa shule dhidi ya Covid-19

Viongozi wa kidini wataka fursa ya kutakasa shule dhidi ya Covid-19

Na TITUS OMINDE

VIONGOZI wa dini kutoka Uasin Gishu wanataka kupewa nafasi ya kutaksa shule kabla ya kufunguliwa.

Ili kufanikisha maombi yao, wametaka serikali iruhusu kufunguliwa kwa makanisa na maeneo mengine ya ibada kabla ya kufungua shule.

Kulingana na viongozi hao, hatua hiyo itawapa nafasi ya kutakasa shule kabla ya kufunguliwa tena baada ya kufungwa kutokana na janga la Covid-19.

Walisema shule nyingi nchini zinadhaminiwa na makanisa na taasisi zingine za kidini kwa hivyo wafadhili lazima wapewe kipaumbele cha kwanza kabla ya kufungua shule kwa utakaso wa mazingira ya kusoma.

Viongozi hao walisema ufunisi wa kufungua makanisa kwanza utakuwa kigezo muhimu cha kubaini iwapoa serikali iko tayari kufungua shule.

Wakiongozwa na Kasisi Bonface Simani wa makanisa ya Bread of Life in Kenya, walisema ikiwa serikali itafanikiwa kufungua tena makanisa, wazazi watakuwa na imani na uwezekano wa serikali kufungua shule na kuweka mazingira bora kwa wanafunzi.

Hata hivyo, walitahadharisha serikali dhidi ya kutumia watoto kama jaribio la uwezo wa serikali kukabiliana na virusi vya corona katika maeneo ya umma.

“Watoto wetu ni dhaifu; serikali inapaswa kuwa angalifu zaidi wakati wa ufunguzi wa shule. Kufunguliwa kwa shule lazima kutanguliwe na ufunguzi wa makanisa ili kuomba na kusafisha madarasa na shule kwa jumla,” alisema Kasisi Simani.

Wachungaji hao waliiomba serikali kuhakikisha kuwa kuna miundombinu ya kutosha kwa kuzingatia sheria za kukabiliana na Covid-19.

Akiongea wakati akikabidhi msaada wa chakula kwa wazazi zaidi ya 100 kutoka Shule ya Comido katika mtaa wa Huruma mjini Eldoret, Kasisi huyo alisema ni makosa kwa serikali kufungua migahawa kabla ya kufungua makanisa na misikiti.

Msimamo wake uliungwa mkono na baraza la maimamu na wahubiri (CIPK) ukanda wa North Rift ambalo mwenyekiti wake ni Sheikh Abubakr Bini

You can share this post!

Walionaswa na kamera za CCTV wakitekeleza wizi kimabavu...

Majambazi watatu wabambwa Siaya

adminleo