• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 5:23 PM
Uteuzi wa Macharia TSC wapingwa kortini

Uteuzi wa Macharia TSC wapingwa kortini

Na BRIAN WASUNA

TUME ya Huduma kwa Walimu (TSC) imeongeza kipindi cha kuhudumu cha katibu wake Nancy Macharia kwa miaka mitano, hatua ambayo imepingwa kortini na wanaharakati.

Katika kesi iliyowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Nakuru, shirika la Midrift Human Rights Network linataka Jaji Monica Mbaru kuamua kwamba hatua ya kuongeza muda wa kuhudumu wa Bi Macharia ni kinyume cha sheria.

Shirika hilo linasema TSC haikuonyesha ushahidi kwamba ilitangaza nafasi ya katibu kuwa wazi.

Muda wa kuhudumu wa Bi Macharia ulimalizika Jumanne lakini TSC imeamua kumuongezea miaka mitano zaidi.

Alhamisi, Chama cha Wanasheria Nchini Kenya (LSK) kilimwandikia barua Mwanasheria Mkuu Kihara Kariuki, kikionya dhidi ya kukiuka sheria katika uteuzi wa katibu wa TSC.

“Tumejua kuna mipango ya kuongeza muda wa kuhudumu wa katibu kwa miaka mitano bila kufuata utaratibu wa kisheria,” mwenyekiti wa LSK Nelson Havi akasema.

You can share this post!

TAHARIRI: Serikali isisahau mazao mengine

WANGARI: Serikali itie bidii katika azimio lake jipya la...

adminleo