Habari Mseto

Wauguzi Kisumu kurejea kazini wakilipwa mishahara

June 26th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA ELIZABETH OJINA

Maafisa wa afya wa Kaunti ya Kisumu wameamua kukatiza mgomo wao na sasa wamepanga kurejea kazini Ijumaa baada ya maagizo ya korti.

Jaji wa mahakama ya leba George Nduma Nderi aliagiza korti itekeleze kupandishwa kwa vyeo kabla ya Julai 3o, 2020 la sivyo wafanyakazi watalazimika kugoma tena.

Katibu wa chama cha wauguzi eneo hilo Maurice Opetu alisema amri hiyo imejiri baada ya kilio cha umma kuhusu kuzorota kwa sekta ya afya kaunti hio.

Maafisa hao wa afya walitisha kwamba wataweka mgomo tena kama serikali ya kaunti hiyo haitatii amri ya korti.

“Hatutakubali na tutaendelea kugoma hadi pale tutalipwa shilingi ya mwisho,” alisema Bw Opetu.

Katibu wa muugano wa maafisa wa afya kaunti ya Kisumu Craus Okumu alionya serikali ya kaunti dhidi ya kutisha wauguzi.

“Wenzetu wako wako huru kurudi kazini lakini tutachunguza kama kuna yeyote atatishwa. Hatuchukulia kwa urahisi kama serikali ya kaunti inataka kutuchezea mchezo wa paka na panya,”alisema Okumu.

Serikali ya Gavana Anyang Nyongo ilikuwa imewashatki kwa kuendesha mgomo.

Maafisa hao wa afya waliweka mgomo wakilalamikia kucheleweshwa kwa misharaha, kutokuepo kwa marupurupu ya corona na kutopandishwa vyeo.

Hii ni mara ya nne maafisa hao wa afya kugoma mwaka huu.

Tafsiri: Faustine Ngila