• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 11:13 AM
KRA kuzindua mfumo mpya wa kodi Nairobi

KRA kuzindua mfumo mpya wa kodi Nairobi

Na COLLINS OMULO

MAMLAKA ya Ushuru Nchini (KRA) itaanzisha mfumo mpya kiteknolojia utakaotumika katika ukusanyaji mapato ya Kaunti ya Nairobi.

Mfumo huo mpya unalenga kuimarisha mapato ambayo yamekuwa chini kwa muda mrefu.

Kulingana na KRA, mbinu hiyo ya ukusanyaji mapato itazinduliwa kwa awamu kwa lengo la kutimiza mahitaji ya kaunti na kushughulikia changamoto ambazo zimeathiri shughuli hiyo kwa miaka mingi.

“Mfumo huo umekuwa ukiandaliwa na kundi la wataalamu katika makao makuu ya KRA kwa kujumuisha maoni kutoka kwa wahusika wote. Kundi hili tayari limekamilisha kazi zote na sasa mfumo huo mpya utaanza kutekelezwa mwezi huu wa Julai kwa awamu,” KRA ikasema kwenye ripoti yake.

KRA ilisema mfumo wa sasa umepitwa na wakati na itakuwa vigumu na ghali kuuimarisha. Vile vile, teknolojia hiyo inaweza kuvurugwa na wahalifu.

KRA pia inasema kuwa shughuli ya ukusanyaji ushuru katika Kaunti ya Nairobi imekumbwa na changamoto nyingi ikiwemo uwezekano wa kutatizwa na wafanyakazi na wateja.

Kwa hivyo, mfumo mpya kukusanya mapato utashirikisha vipengele vingi kama mitambo ya kuwawezesha wateja kulipa ushuru kupitia apu za simu ya mkono au mitandaoni.

You can share this post!

Bidcoro yazindua sharubati aina ya SunQuick

Manaibu gavana waomba wapewe kazi za kufanya

adminleo