• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Mumias Sugar yaagiza vifaa vipya

Mumias Sugar yaagiza vifaa vipya

BENSON AMADALA na FAUSTINE NGILA

Kampuni ya Mumias imeangiza vifaa vipya vya kusaidia Mumias kusaga sukari kwenye kiwanda. 

Mkurugezi wa kiwanda cha sukari Bw Ponangiplli Venkata Ramana Rao alisema kwamba vifaa hivyo vitatolewa Afrika Kusini na kuletwa humu nchini kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Mipango ya kuagiza vifaa hivyo ilichelewa kwa sababu ya vikwazo vilivyowekwa kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa virusi vya corona.

Bw Rao hakutaja bei ya vifaa hivyo. Watakaovitumia kusaga sukari walivichunguza kwenye kiwanda na kusema viko tayari kufanya kazi.

Bw Rao alisema kwamba kisiagi hicho kinatarajiwa kuanza kazi  mwezi Septemba.

“Tulikuwa tunatarajia kufanya matayarisho ya kusaga sukari haraka lakini kumekuwa na matatizo yaliyochelewesha shughuli hiyo.

“Tunatarajia vifaa hivyo kufika mwishoni wa mwezi huu ndio tuweze kuifanyia majaribio,”alisema Bw Rao.

Kisiagi hicho kwa sasa kinatumika kutengeneza sukari lakini shughuli hiyo inachelewa kwa ukosefu wa sukari nguru.

You can share this post!

Uagizaji wa sukari kutoka nje wapigwa marufuku

Waluke aomba aruhusiwe kushiriki mijadala ya bunge kwa Zoom...

adminleo