• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 1:47 PM
Maafisa wakuu wapya wateuliwa kaunti ya Kiambu

Maafisa wakuu wapya wateuliwa kaunti ya Kiambu

Na LAWRENCE ONGARO

GAVANA wa Kiambu Dkt James Nyoro, amewateua maafisa wakuu wapya watakaoendesha shughuli za kaunti hiyo.

Wakati wa uteuzi huo aliwataka maafisa hao wawe kielelezo na waweke taswira nzuri itakayoigwa na wafanyakazi wengine.

Kulingana na uteuzi huo Bi Jennifer Musyoki ni afisa mkuu msimamizi wa idara ya maji.

Bi Mary Njoroge ni afisa mkuu wa utalii na uwekezaji.

Bw Peter Ndegwa ni afisa mkuu wa ushirika na maendeleo. Naye George Thuku, ni afisa mkuu ambaye ni msimamizi wa kaunti mzima.

Bw Frankline Wambugu, ni afisa mkuu wa mawasiliano na uhusiano mwema wa umma.

Dkt Patrick Njeru Nyaga ni afisa mkuu wa afya katika kaunti hiyo.

Bw Zacharia Karanja ni afisa wa biashara na viwanda. Bw Charles Njuguna ni mkuu wa maswala ya umma.

Bw Edward Njihia ni afisa wa mazingara na maswala ya taka.

Dkt Nyoro alihimiza kila afisa afanye kazi yake kwa ukakamavu bila mapendeleo.

“Ninawataka muwe maafisa wenyewe maono kwa kuhakikisha kaunti ya kiambu itakuwa katika ramani ya Kenya,” alisema Dkt Nyoro.

Alisema kila afisa atapewa nafasi kufanya kazi yake bila kuingilia na yeyote.

“Kila mmoja amepewa nafasi kuonyesha ujuzi wake ambapo wananchi wanangoja kutambua ujuzi huo,” alisema Dkt Nyoro.

Alisema tayari Kaunti ya Kiambu imeweka mikakati kabambe jinsi itakavyoendesha miradi yake.

Alisema kwa wakati huu maswala muhimu yanayolengwa ni miradi ya maji, barabara, na umeme.

Bw Frankline Wambugu, afisa mkuu wa mawasilianao na uhusiano mwema, alisema ataboresha idara hiyo ili kuafikia malengo yake.

“Ninashukuru kupewa wadhifa huo ambao una ushindani mkali. Nitahakikisha idara hiyo inatekeleza wajibu wake ipasavyo,” alisema Bw Wambugu.

You can share this post!

Joho awaonya vijana wanaohangaisha wakazi Mombasa

ONYANGO: Corona imefifisha zaidi umoja Afrika Mashariki

adminleo