• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 12:04 PM
Ruto apuuza mpango wa kusukuma Raila Ikulu

Ruto apuuza mpango wa kusukuma Raila Ikulu

WANDERI KAMAU NA DPPS

NAIBU Rais William Ruto amepuuzilia mbali viongozi wanaotishia kwamba kikundi cha washawishi wa kitaifa katika Ikulu ndicho kitaamua atakayemrithi Rais Uhuru Kenyatta ifikapo 2022.

Akizungumza Jumanne nyumbani kwake Karen, Kaunti ya Nairobi, Dkt Ruto alisisitiza kuwa haogopi vitisho ambavyo vimekuwa vikiendeshwa dhidi yake pamoja na wandani wake kutokana na azma yake kuwania urais.

Dkt Ruto alisema kuwa hali ambayo yeye anapitia ni sawa na ilivyokuwa kabla ya 2013, ambapo Wakenya walionywa dhidi ya kumchagua yeye na Rais Uhuru Kenyatta kutokana na mashtaka yaliyowakabili katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Alikuwa akiwahutubia viongozi kadhaa kutoka Kaunti ya Kajiado waliomtembelea.

“Kama ningekuwa mtu mwoga hatungeunda serikali ya Jubilee. Tulikuwa tunatishiwa mambo mengi. Ni sawa na vile tunaambiwa hata saa hii.

“Tunatishwa eti kuna watu watatuibia kura hata mkipiga namna gani na eti kuna watu wameketi mahali fulani wataamua. Mimi nataka niwaambie, hao watu tunawangojea. Watakuja na ‘system’, sisi tutakuja na wananchi na Mungu. Na tutaona vile hii kazi itaendelea,” akasema Dkt Ruto.

Wiki chache zilizopita, Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt Oburu Oginga, alieleza kuwa kakake Raila Odinga, atasaidiwa kufika Ikulun2022 na washawishi walio katika Ikulu.

Wikendi Naibu Mwenyekiti wa Jubilee, David Murathe alidai kuna mipango ya kumsukuma Bw Odinga awe Rais 2022.

Bw Odinga amekuwa akikwepa kutangaza kama anapanga kuwania urais tena na badala yake husema huu ni wakati wa kuendeleza nchi.

You can share this post!

Mjadala wa fedha waingizwa ukabila

Wakazi wa Kingoro waandamana malalamiko yakiwa ni...

adminleo