• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 9:55 AM
KICD kuwanoa walimu kidijitali

KICD kuwanoa walimu kidijitali

NA FAUSTINE NGILA

TAASISI ya Kitaifa ya Kuandaa Mitaala (KICD) imeanzisha mpango wa kuwanoa walimu kidijitali kama mojawapo ya mbinu za kuimarisha elimu ya kisasa.

Kwenye mradi huo, KICD imeshirikiana na kampuni za Microsoft na Safaricom kuwapa walimu uelewa na ujuzi wa kuwafundisha wanafunzi matini kwa njia ya kidijitali katika kipindi hiki ambapo teknolojia imegeuza jinsi sekta nyingi zinaendesha shughuli kutokana na janga la corona.

“Mafunzo haya hayatalipishwa na yatafanyika kupitia mitandao kwa kundi la kwanza kama majararibio kabla ya kutekelezwa kote nchini,” akasema Dkt Joel Mabonga, naibu mkurugenzi wa KICD.

KICD pia imeboresha studio zake za kuepeperusha makala ya elimu kupitia runginga ya Edu TV ambayo ndiyo pekee nchini inawapa wanafunzi masomo wakati huu shule zimefungwa.

Studio hizo zimeundwa kwa kutumia mionekano mbalimbali ili kuwiana na wanafunzi katika ngazi tofauti za masomo.Kwa wanafunzi wa elimu ya msingi, mwonekano una miundo tofauti ili kushirikisha fikra za wanafunzi na kuhakikisha wamesikiza kinachofundishwa.

You can share this post!

Polisi wazima mkutano wa Mudavadi mjini Mbale

NGILA: Tahadhari, msimu wa habari feki na kuumbuana ndio...