• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Hatima ya ziara ya Ruto kesho bado haijulikani

Hatima ya ziara ya Ruto kesho bado haijulikani

Na SHABAN MAKOKHA

HALI ya sintofahamu imegubika ziara ya Naibu Rais Dkt William Ruto katika eneo la Magharibi, baada ya polisi kukosa kutoa kibali kwa waandalizi wa hafla hiyo, siku mbili kabla ya siku iliyopendekezwa ya mikutano.

Dkt Ruto anatarajiwa kuongoza shughuli mbili za kanisa siku ya Jumapili katika maeneo bunge ya Mumias na Matungu mtawalia.

Wafuasi wa Ruto kutoka mkoa huo wanajiandaa kwa ziara yake ya kuchangisha pesa kwa parokia ya St Leo huko Shianda kaunti ndogo ya Mumias Mashariki na Our Lady of Assumption Indangalasia huko Matungu baada ya hafla hizo kufutwa Oktoba 11, 2020.

Wafadhili wamekwama baada ya msimamo wa maafisa wa polisi wanaotaja tishio la usalama na kutozingatia maagizo ya Covid-19 kama sababu kuu ya kukosa kupeana kibali.

Afisa mkuu katika kituo cha polisi cha Shianda Bw Christopher Wesonga, alisema mnamo Oktoba 10 aliwaandikia barua waandalizi wa shughuli hiyo akiwajulisha kuwa uchangishaji huo ulisimamishwa kwa sababu ya maagizo kutoka kwa afya ya umma kuhusu Covid-19.

Kupitia barua kwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Kanisa Katoliki la St Leo, Bw Wesonga aliiarifu kamati hiyo kwamba hakutakuwa na misa takatifu inayojumuisha makanisa yote kumi ya katoliki yaliyo chini ya parokia ya Bumini ambayo inamiliki mamlaka ya eneo lote la Mumias Mashariki.

“Sote tunajua hakupaswi kuwa na aina yoyote ya mkusanyiko karibu na kanisa lililotajwa. Mkutano wowote utakaoendeshwa utakuwa ukiukaji wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Amri ya Umma Sura ya 56 ya Kenya na haitavumiliwa,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

Mawasiliano sawia kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Matungu Bernard Ngungu yalifikishwa kwa waandalizi katika parokia ya Indangalasia.

Bw Ngungu alisema polisi walikuwa wamekusanya ripoti za ujasusi zinazoonyesha kuwa watu wengine walikuwa wanapanga kusababisha machafuko katika mkusanyanyiko wa ugavi wa hela.

“Kwa kuongezea, vizuizi vya Covid-19 bado vinatumika na hii ilichangia kupigwa marufuku kwa hafla hiyo ambayo ingekusanya mamia ya watu pamoja,” akasema Bw Ngungu.

Kikosi cha maafisa wa polisi kimetua katika maeneo bunge kuzuia jaribio lolote la wanasiasa wanaoshirikiana na Dkt Ruto kufikia makanisa hayo mawili kwa hofu kwamba wataenda kinyume na maagizo ya polisi.

Mbunge wa Mumias Mashariki Benjamin Washiali alisema watakagua mikutano hiyo na kupanga siku nyingine.

You can share this post!

Balozi azirai na kufariki ghafla akiwa benki

Manaibu wa magavana sasa kupata sauti BBI ikipita