• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:05 AM
Iweje kaunti zinatumia 70% ya bajeti kulipa mishahara pekee?

Iweje kaunti zinatumia 70% ya bajeti kulipa mishahara pekee?

Na BERNARDINE MUTANU

Kaunti zimeendelea kutumia pesa zaidi kulipa mishahara na marupurupu kulingana na ripoti mpya kutoka kwa Mdhibiti wa Bajeti.

Data ya miezi sita kutoka Desemba inaonyesha kuwa kaunti zilitumia asilimia 70 ya bajeti zao kulipa mishahara.

Mdhibiti wa bajeti Bi Agnes Odhiambo alisema kiwango cha matumizi hayo ni Sh66.4 bilioni kutoka Sh61.8 bilioni katika kipindi hicho mwaka jana,

Hicho ni kiwango cha juu zaidi cha matumizi ya bajeti kulipa mishahara tangu ugatuzi kuanza kutekelezwa.

Kiwango hicho kimezidishwa na ongezeko la marupurupu kwa wafanyikazi wa kaunti ambapo Kaunti ya Tharaka Nithi iliongoza kwa asilimia 94.4 ya matumizi ya pesa kwa marupurupu na kufuatwa na Meru kwa asilimia 92.5 na Embu kwa asilimia 86.5, alisema mdhibiti huyo.

Lakini Nairobi ilitumia pesa nyingi zaidi(Sh6.63 bilioni) na kufuatwa na Kakamega(Sh2.69 bilioni na Kiambu(Sh2.46 bilioni).

You can share this post!

Marufuku ya ukataji miti yaongezwa kwa miezi 6

SoNy Sugar yatimua wachezaji 4 licha ya kuburuta mkia ligini

adminleo