• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 5:55 AM
Mzee Makanyaga azikwa katika makaburi ya Kariorkor

Mzee Makanyaga azikwa katika makaburi ya Kariorkor

NA PETER CHANGTOEK

Aliyekuwa mwigizaji maarufu, Mohammed Tajiri, almaarufu Mzee Makanyaga, amezikwa katika makaburi ya Kariorkor, mnamo siku ya Jumatano adhuhuri.

Makanyaga aliaga dunia katika eneo la Majengo, Pumwani, Nairobi, siku ya Jumanne, akiwa na umri wa miaka themanini na mitano (85).

Alikuwa mwigizaji maarufu katika vipindi kadha wa kadha, ambavyo vilikuwa vikipeperushwa hewani katika Shirika la Utangazaji la Kenya, KBC, wakati huo likijulikana kama Sauti ya Kenya (Voice of Kenya).

Kwa mujibu wa wale waliokuwa wametagusana naye ni kwamba, Makanyaga alikuwa na kipaji cha ucheshi.

Kwa mujibu wa Bi Mary Khavere, almaarufu Mama Kayai, Makanyaga alikuwa mkarimu na angemsaidia yeyote ambaye angeuhitaji usaidizi wake.

“Kuna wakati ambapo tulikuwa tukicheza densi asilia katika kilabu kimoja kilichokuwa kikijulikana kwa jina Black Golden Stars, kabla hatujaanza safari ya kuigiza,” akafichua Mama Kayai, ambaye alikuwa ametagusana naye kwa muda mrefu.

Miongoni mwa vipindi ambavyo marehemu alikuwa akiigiza kwavyo ni Vitimbi, Vioja Mahakamani, Darubini, Zuberi na Chipukizi.

Mamia ya waombolezaji walikusanyika nyumbani kwake, kabla hajazikwa katika eneo la Kariorkor makaburini.

Miongoni mwa wale waliohudhuria maziko ya mwendazake ni pamoja na mwigizaji Mathias Keya, almaarufu Alfonse Dot Makacha Makokha.

You can share this post!

ABIGAIL KAVISA: Ndoto yangu katika ucheshi ni kufikia upeo...

Umuhimu wa kuwa na ukomavu kukabili mahangaiko ya dunia