• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 7:55 PM
ODM yaanza kuongea na Obado baada ya kushindwa kumtimua

ODM yaanza kuongea na Obado baada ya kushindwa kumtimua

Na Charles Wasonga

GAVANA wa Migori Okoth Obado Alhamisi alikutana na uongozi wa ODM majuma mawili baada ya juhudi za chama hicho kumwondoa mamlakani kugonga mwamba.

Hii ni baada ya madiwani wa 41 wa ODM katika bunge la Kaunti ya Migori kugawanyika kuhusu mpango huo uliosukumwa na uongozi wa chama hicho.

Kwenye taarifa jana, Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna alisema walijadiliana kuhusu jinsi ya kuendeleza shughuli za serikali ya Migori kwa hali ilivyo sasa.

Mahakama imemzuia Gavana huyo kuingia afisini baada ya kushtakiwa kwa wizi wa Sh73 milioni, pesa za Serikali ya Kaunti ya Migori akishirikiana na wanawe wanne. Bw Obado na wanawe waliachiliwa kwa dhamana ya jumla ya Sh8.7 milioni, pesa taslimu baada ya kukanusha mashtaka.

“Katika mkutano huo, pia ilikubalika kwamba mashauriano zaidi yafanywe na wadau wengine kama vile Bunge la Kaunti ya Migori a tawi la Migori la chama cha ODM,” akaongeza Bw Sifuna.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo wa jana katika makao makuu ya ODM, Nairobi ni mwenyekiti wa kitaifa John Mbadi, Timothy Bosire (Mweka hazina), Abdikadir Aden (Katibu mtendaji) na Mkurugenzi wa Masuala ya Kisiasa Opiyo Wandayi.

You can share this post!

Miradi ya barabara hatarini Mombasa

DAISY: Wanawake waridhike na maumbile, wasijiumbue