• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Kang’ata kurai Seneti ipitishe mswada wa chai

Kang’ata kurai Seneti ipitishe mswada wa chai

Na MWANGI MUIRURI

KIRANJA wa Seneti Irungu Kang’ata ameahidi kuwashawishi maseneta waidhinishe Mswada wa Chai akisema utawafaidi pakubwa wakulima wa zao hilo.

Kulingana naye, sheria hiyo inampa waziri wa Kilimo uwezo wa kutekeleza mageuzi ambayo yatachangia kuongezeka kwa mapato ya wakulima.

Bw Kang’ata alikuwa akimjibu Mbunge wa Gatanga, Nduati Ngugi ambaye alilitaka Bunge la Seneti kuidhinisha mswada huo haraka ili wakulima waanze kufaidi kuanzia mwaka 2021.

Wiki jana, kiongozi wa ODM, Raila Odinga aliwasifu wabunge kwa kupitisha mswada huo uliodhaminiwa na Seneta wa Kericho, Aaron Cheruiyot.

Bw Odinga alisema hatua hiyo ya Bunge la Kitaifa sasa inampa Waziri Peter Munya nafasi ya kufanikisha mageuzi katika sekta ya majani chai nchini.

Kiongozi huyo wa upinzani pia aliahidi kuwashawishi maseneta kuidhinisha mswada huo ili utiwe saini kuwa sheria.

Wakulima sasa wana matumaini ya kufaidika kutokana na kazi yao.

You can share this post!

Wanafunzi walalamikia mmoja wao kunajisiwa

Afya: Kilio serikali zajikokota kusaidia