• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 11:16 AM
Wagonjwa wa kansa wageukia mitishamba

Wagonjwa wa kansa wageukia mitishamba

Na BARNABAS BII

WAGONJWA wa kansa ambao hawamudu gharama ya matibabu katika hospitali za kibinafsi sasa wanatumia dawa za kienyeji wakisubiri huduma katika hospitali za umma kurejelewa.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, maelfu ya Wakenya wanaougua kansa hufariki kila mwaka kutokana na gharama ya juu ya matibabu katika hospitali za kibinafsi.

“Kuna ongezeko la visa vipya vya kansa na mengi yanastahili kufanywa ili kuzuia ugonjwa huo,” akasema Dkt Naftali Busakhala, mtaalamu wa matibabu ya kansa katika Hospitali ya Eldoret.

Takwimu za wizara ya Afya zinaonyesha kuwa asilimia saba ya vifo humu nchini husababishwa na kansa. Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi (MRTH) iliyoko Eldoret, imelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa wa kansa.

Kulemewa

Hospitali hiyo ya rufaa ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 500 pekee. Lakini idadi ya wagonjwa wa kansa ni kubwa zaidi kwani inahudumia watu kutoka maeneo ya Bonde la Ufa, Magharibi, Nyanza, Mlima Kenya na hata Uganda.Dkt Wilson Aruasa, Mkururugenzi Mkuu wa MRTH, anasema gharama ya juu ya matibabu ya kansa inafanya wagonjwa wasiomudu kutafuta matibabu mbadala.

Matibabu ya kansa hutolewa kwa hatua sita na kila hatua hugharimu kati ya Sh5,000 na Sh10,000. Kwa mujibu wa Taasisi ya Kitaifa kuhusu Kansa, visa vipya 47,887 hurekodiwa kwa mwaka na vifo 32,987 vinavyotokana na ugonjwa huo hutokea kila mwaka.Watu 133 hupatikna na maradhi hayo kila siku, kulingana na taasisi hiyo.

Wakenya 90 hufariki kutokana na kansa kila siku.Dkt Aruasa anasema kuwa idadi hiyo kubwa ya vifo husababishwa na watu kuenda kupimwa wakiwa wamechelewa na ukosefu wa fedha za matibabu kutokana na umaskini.

You can share this post!

Treni kufufua uchumi Mlima Kenya

Wanasiasa wakosa adabu mazikoni