• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 6:55 AM
KILIMO: Bonde la Ufa lajitosa kwa ukuzaji kahawa huku Kati ikitamauka

KILIMO: Bonde la Ufa lajitosa kwa ukuzaji kahawa huku Kati ikitamauka

Na CHARLES WASONGA

ENEO la Rift Valley linaibuka kama kiongozi katika uzalishaji kahawa huku kilimo cha zao hilo kikififia katika eneo la Kati mwa Kenya.

Hii ni kwa sababu wakulima wengi katika eneo la Kati sasa wanawekeza sana katika miradi ya ujenzi wa nyumba za kibiashara badala ya kilimo cha kahawa.

Wakulima wengi katika eneo la Rift Valley sasa wanakumbatia kilimo cha kahawa kama chanzo cha mapato kando na majani chai, mahindi na ngano kufuatia ongezeko la hitaji la kahawa katika masoko ya ng’ambo.

Hali hii inachangiwa na kupungua kwa uzalishaji wa kahawa katika mataifa ya kigeni ambayo huzalisha zao hilo kwa wingi.

Kulingana na  ripoti ya Wakfu wa Utafiti kuhusu Kahawa (CRF) , uzalishaji wa kahawa ulipungua katika eneo la Kati katika msimu uliopita kutokana na hali mbaya ya anga.

Kwa mfano, uzalishaji kahawa katika kaunti ya Nyeri ulipungua kutoka kilo 35,902,046 hadi  kilo 21,060, 572 na kupelekea wakulima kupata hasara kubwa.

Wakulima wanadai kando na hali mbaya ya anga, walipata hasara kwa sababu ya kushuka kwa bei ya zao hilo katika masoko ya humu nchini na kimataifa.

“Hali ya anga katika maeneo ya Rift Valley kunakokuzwa kahawa ni nzuri ikilinganishwa na maeneo mengine humu nchini. Ardhi pia ina rotuba bora kwa kahawa,” ikasema ripoti ya CRF.

Eneo la Rift Valley lilizalishwa tani 65,618.50 ya kahawa katika msimu uliopita ikilinganishwa na tani 19,573.38 katika msimu uliotangulia kwa sababu wakulima wengi waliwekeza katika upanzi wa mmea huu.

Kufuatia hali hiyo, wakfu wa CRF iliimarisha uzalishaji wa aina mbalimbali za mbegu za kahawa ili kuwezesha wa kupata mbegu hizo kwa gharama nafuu.

Kahawa hupandwa kwa wingi katika kaunti za Uasin Gishu, Trans Nzoia, Baringo katika eneo la North Rift na Kericho na Bomet katika eneo la South Rift. Zao hilo pia hupandwa katika sehemu mbalimbali katika kaunti ya Nakuru.

Kilimo cha kahawa kimepigwa jeki na hataua ya serikali ya kuitengea  sekta hiyo Sh81 milioni na Hazina ya Ustawi wa Kilimo cha Kahawa (CDF) na Sh15 milion kupitia Benki ya Ushirika mwaka ujao. Fedha hizi zimewatia shime wakulima hali ambayo imewafanya kupanua ekari za mashamba ya kahawa.

Kulingana na CRF, hitaji la miche ya kahawa imepanda kwa kima cha asilimia hali iliyopelekea miche 6 milioni kusambazwa kabla ya msimu wa upanzi Oktoba mwaka 2017.

“Utayarishaji wa miche umeimarishwa ili kupiga jeki uzalishaji wa kahawa katika eneo la Rift Valley,” ikaeleza ripoti hiyo ambayo ilitolewa mwezi Machi 2018.

You can share this post!

Wabunge wamtaka Rais kuwasimamisha kazi mawaziri na...

Afisi ya DPP yachunguzwa kwa ulaji rushwa

adminleo