• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 4:31 PM
Mkurugenzi kizimbani kwa kughushi stempu za KEBS

Mkurugenzi kizimbani kwa kughushi stempu za KEBS

Na RICHARD MUNGUTI

MKURUGENZI wa kampuni moja ya kutengeneza vyakula alishtakiwa Ijumaa kwa kuweka stempu ya shirika la ukadiriaji ubora wa bidhaa (KeBS) katika bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Sh1.milioni bila idhini.

Bw Rajan Ramesh Malde , wa kampuni ya Trufoods alifikishwa katika Mahakama ya Milimani , Nairobi mwendo wa saa nne na maafisa wa Polisi walioandamana na maafisa wa KeBS.

Alikanusha shtaka la kuweka stempu ya KeBS katika mikembe ya Zesta yenye kilo 4,437 za Njugua karanga iliyosiagwa yenye thamani ya Sh350,487.

Hakimu mkazo Bi Miriam Mugure , alielezwa mshtakiwa aliweka stempu nyingine kwenye kilo 14,790 katika mikebe na pakiti za Chocolate yenye thamani ya Sh1,036,482.

Upande wa mashtaka ulio ongozwa na Bi Sarah Ada ulisema maafisa wa KeBS walipata mashtakiwa ameweka stempu kwenye kilo 1,565 za mikebe  ya rojo la nyanya yenye thamani ya Sh319,639.

Bi Ada alisema jumla ya thamani ya bidhaa zilizowekwa stempu  hizo ni Sh1,706, 217.

Mahakama ilifahamishwa kuwa  maafisa wa KeBS walisema stempu hizo ziliwekwa kwenye bidhaa hizo bila idhini yao.

Bi Mugure alielezwa sheria inawataka wenye makampuni ya kutengeneza bidhaa ama kuigiza bidhaa wahakikishe zimekaguliwa kubaini ikiwa zafaa kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

Mshtakiwa aliomba aachiliwe kwa dhamana.

Bi Ada hakupinga ombi la mshukiwa huyo wa kuuza bidhaa zilizowekwa stempu ya KeBS kinyume cha sheria.

Hakimu alimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh100,000 pesa tasilimu hadi Julai 17 kesi itakaposikizwa.

Mshtakiwa alidaiwa alikutwa ameweka stempu hizo mnamo Juni 7, 2018 katika kiwanda chake kwenye barabara ya Jogoo Nairobi.

Alitiwa nguvuni na kufikishwa kortini moja kwa moja.

You can share this post!

Wachina wahukumiwa kufagia mahakama

Polisi pabaya kwa mauaji ya mwanamke City Park

adminleo