• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Morocco sasa yaangazia kuandaa Kombe la Dunia 2030

Morocco sasa yaangazia kuandaa Kombe la Dunia 2030

Na GEOFFREY ANENE

MOROCCO bado ina matumaini ya kuandaa Kombe la Dunia siku moja hata baada ya juhudi zake kugonga mwamba mara tano.

Saa chache baada ya ombi lake la kuwa mwenyeji wa makala ya mwaka 2026 kufeli, Serikali ya Morocco ilitangaza kwamba itawania haki za kuwa mwenyeji wa mwaka 2030. Ilijaribu bila mafanikio kuwa mwenyeji mwaka 1994, 1998, 2006, 2010 na 2026.

Morocco ilijitosa uwanja kupambana na ombi la pamoja la Amerika Kaskazini (Marekani, Canada na Mexico) la mwaka 2026, lakini ikapoteza kwa kura 134-65 Juni 13, 2018 jijini Moscow nchini Urusi.

Tovuti ya Morocco World News sasa imeripoti kwamba Waziri wa Michezo Rachid Talbi Alami ametangaza kwamba nchi hiyo haitakufa moyo na itagombea kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la mwaka 2030.

Imeongeza kwamba Talbi amesema Morocco itaendelea na miradi yake ya mwaka 2026 jinsi ilivyopangwa. “Matarajio ni kwamba kukamilisha miradi ya mwaka 2026 itaweka Morocco pazuri kwa sababu itakuwa na nguvu zaidi na kuwa na ombi lililo zito kushindania kuwa mwenyeji wa mwaka 2030,” lilisema.

Inasemekana Waziri huyu alipata maagizo kutoka kwa Mfalme wa Morocco, Mohammed, ambaye anataka taifa hilo liendelee kuweka hai ndoto ya kuandaa fainali hizo.

You can share this post!

Ni kicheko tu kwa Morocco kuona Saudia ikinyeshewa 5-0 na...

Mtaalamu aonya dhidi ya kuharakisha kupyesha mtaala

adminleo