• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 11:13 AM
Akiri amechinja paka 1,000 kuuzia nyama waundaji wa sambusa tangu 2012

Akiri amechinja paka 1,000 kuuzia nyama waundaji wa sambusa tangu 2012

NA PETER MBURU

POLISI mjini Nakuru wanamzuilia mwanamume ambaye anatuhumiwa kuendeleza biashara ya nyama ya paka kwa wauzaji wa samosa, baada yake kukamatwa akimchinja mnyama huyo Jumapili.

Bw James Mkangu Kimani (pichani) alikiri kuwa amewachinja Zaidi ya paka 1,000 kwa wauzaji hao na hoteli Fulani mjini tangu alipoanza biashara hiyo mwaka wa 2012.

Alisema alianza biashara hiyo baada ya kubaini pengo sokoni, japo akiongeza kuwa wateja wake hawafahamu kuwa nyama wanayoila ni ya paka.

Lakini mtuhumiwa alieleza waandishi wa habari kuwa ana soko ya nyama na ngozi ya mnyama huyo, akisema kwa kila paka mmoja anapokea Sh500.

“Nilianza biashara hii 2012 nilipoona kuna upungufu wa nyama kwa wauzaji wa samosa. Huwa nawaeleza wateja wangu kuwa Napata nyama kutoka eneo la Gioto lakini hawafahamu ni yap aka,” akasema Bw Kimani.

James Mkangu Kimani aelezea jinsi amewachinja zaidi ya paka 1,000 na kuuza kwa wauzaji wa nyama na wamiliki wa hoteli moja mjini tangu alipoanza biashara hiyo 2012. Picha/ Peter Mburu

Alikamatwa katika eneo la reli alipokuwa akimchinja mmoja wa wanyama hao. Alikuwa tayari amemkata shingo na alikuwa kwenye shughuli za kumnywafua ngozi.

Wakazi ambao walivutiwa na tukio hilo lisilo la kawaida walieleza hofu yao haswa baada ya kutambua kuwa huenda wakawa wamekula nyama hiyo bila kujua. Wakazi hao wenye ghadhabu walitaka kumuua lakini akaokolewa na polisi ambao walipata ufahamu wa tukio hilo kwa haraka na akafungiwa katika kituo cha polisi cha Ukulima.

“Hii inamaanisha kuwa vyakula tunavyotumia haswa mjini ni vya kutiliwa shaka, amesema kuwa ana soko la tayari na kuwa ameuza Zaidi yap aka 1,000. Hili ni jambo la kushtua,” akasema Bw Maina Saitoti.

“Yeyote anayeendeleza biashara hii ya kuwauzia watu paka hafanyi haki,” akasema Paul Asika.

Kulingana na daktari wa mifugo kutoka kaunti ya Nakuru Bw Githui Kaba, tendo hilo ni kinyume na sheria, kwani kula nyama ambayo haijapimwa ama nyama ya mnyama asiyeruhusiwa si salama.

“kulingana na sheria ya kuelekeza ulaji wa nyama na afya ya umma, kula nyama ambayo haijapimwa na daktari ama ya mnyama ambaye haruhusiwi kuwa chakukla si salama. Paka haruhusiwi kuliwa,” akasema daktari huyo.

You can share this post!

URUSI 2018: Ahadi ya pesa ilivyochochea Nigeria kuiyeyusha...

Bado tuko pamoja, Ruto apuuza mpasuko ndani ya Jubilee

adminleo