Kizaa madiwani wakilaumiana kula hongo wazime ripoti
Na NDUNG’U GACHANE
KULIZUKA vita vikali na shutuma za maneno makali miongoni mwa madiwani katika kaunti ya Murangá jana kuhusu kuwasilishwa kwa ripoti ya mpango wa maendeleo ya kaunti (County Intergrated Development Plan).
Mwenyekiti wa kamati ya fedha Kiiru Mbembe, alikataa kuwasilisha ripoti hiyo bungeni akidai hakuwa ameikagua baada ya waziri wa fedha kukataa kutoa mapendekezo yake kuihusu.
Hata hivyo, wanachama wa kamati hiyo walimlaumu Bw Mbembe kwa kuhujumu uwasilishaji wa ripoti hiyo kutokana na maslahi yake ya kibinafsi na kusema walikuwa tayari kuiwasilisha iwapo hangeweza.
Vuta ni kuvute ilianza pale diwani wa Makuyu Stanley Mwangi alipodai kwamba waliokuwa wakiunga mkono ripoti hiyo walihongwa na wakuu wa kaunti kwa kupewa Sh42,000.