• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 7:55 AM
UREMBO: Jinsi ya kujipaka vipodozi msimu wa baridi

UREMBO: Jinsi ya kujipaka vipodozi msimu wa baridi

Na PAULINE ONGAJI

Msimu wa baridi umebisha na kama kawaida sharti mtindo wa maisha kidogo ubadilike. Mapambo pia hayajasazwa kwani hautarajiwi kujipodoa kwa mbinu sawa na unazotumia wakati wa kawaida au kukiwa na jua.

Mbinu hizi zitakusaidia kufanikisha vipodozi vyako wakati huu:

•Nawa uso kwa kutumia bidhaa zilizoundwa kwa viungo vyepesi: Unashauriwa kunawa uso kwa kutumia bidhaa zilizoundwa kwa viungo vyepesi na zilizo na uwezo wa kuondoa vipodozi, kusafisha na kung’arisha ngozi pasipo kuikausha.

•Tayarisha ngozi yako wakati wa usiku: Paka ngozi yako mafuta kwani hii itasaidia kupaka foundation baadaye. Hapa unashauriwa kutumia bidhaa zilizoundwa pia kwa viungo asili ili kuzuia vipodozi kudondoka haraka na mwasho pia, matatizo yanayoshuhudiwa msimu wa baridi. Ikiwa ngozi yako ni aina iliyo na mafuta mengi, unashauriwa kujaribu bidhaa za jeli.

•Tumia primer: Bidhaa hii ni muhimu kwani husaidia kudumisha vipodozi vyako kwa muda mrefu.

•Paka safu chache za vipodozi: Paka safu chache za kila kipodozi unachotumia. Pia unashauriwa kutumia bidhaa zinazofungia unyevu kwenye ngozi.

•Hakikisha macho yako yanang’aa wakati huu: Unashauriwa kuangazia sana vipodozi vya macho kwa kutumia wanja usiopenyeza maji.

•Shughulikia mdomo wako: Tumia bidhaa za kuondoa ngozi iliyokauka kwenye mdomo wako na ujipake lipstiki ya kupendeza na isiyosababisha sehemu hii kukauka.

•Nyunyiza bidhaa ya kudumisha vipodozi usoni (setting spray): Unashauriwa kujinyunyizia bidhaa hii ili kuzuia vipodozi kutapakaa usoni baada ya kujipaka huku ngozi yako ikisalia maridadi mchana kutwa.

You can share this post!

FUNGUKA: Lengo langu ni kupata zaidi ya watoto 9

JUBILEE YATOKOTA: Joto kali huku wandani wa Uhuru na Ruto...

adminleo