Habari Mseto

Wakazi wa mitaa ya mabanda waandamana kupinga ubomoaji

August 8th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na RICHARD MUNGUTI

SHUGHULI katika eneo la Community, Nairobi zilisambaratishwa na maandamano ya wakazi wa mitaa ya mabanda waliofurika kwenye barabara wakipinga kubomolewa kwa makazi yao katika maeneo mbalimbali Jumatano.

Waandamanaji hao  kutoka vitongoji vya Mukuru kwa Njenga , Kileleleshwa , Kwa Reuben, Sinai, Viwandani, Kiambiu na Mathare waliandamana kulalamikia hatua ya  serikali ya kaunti ya Nairobi kubomoa makazi yao.

Waandamanaji hao walisema  katiba imewapa haki ya kumiliki makao na wala hakuna anayepasa kuwazuia  wakiishi wanakoishi “ kwa sasa.”

Katika muda wa siku chache hivi karibuni matingatinga ya kaunti ya Nairobi yamekuwa yakibomoa mitaa ya mabanda na kuwaacha maelfu ya wakazi bila makao.

Wakibeba mabango na fufuzela waandamanaji hao waliziba barabara hata ikawa vigumu kwa magari ya abiria kuelekea hospitali kuu ya Kenyatta (KNH) na Kibera.

Maandamano yaliendelea kutoka saa tatu asubuhi hadi saa tisa.