Mama na mwanawe wakana kuuzia Kenya Power transfoma feki
Na RICHARD MUNGUTI
MAMA na mtoto waliokuwa nchini Uingereza Jumatatu walishtakiwa kwa kashfa ya mauzo ya transfoma feki kwa kampuni ya Kenya Power mitambo ya transfoma feki na kupokea zaidi ya Sh201milioni kinyume cha sheria.
Bi Grace Wanjira na mwanawe John Antony Mungai walikanusha mashtaka matatu dhidi yao walipofikishwa katika Mahakama ya Milimani Nairobi.
Wawili hao walijisalamisha kwa hakimu mkuu mahakama ya kuamua kesi za ufisadi (ACC) Bw Douglas Ogoti baada ya kibali cha kuwatia nguvuni Julai 16, 2018.
Bi Wanjira na mwanawe Antony hawakufika kortini ikidaiwa walikuwa wameenda Uingereza kwa matibabu.
“Wanjiru na Antony wako ulaya kupokea matibabu,” alidokeza wakili Karathe Wandugi mnamo Julai 16.
Lakini jana wakili huyo aliambia korti kuwa Wanjiru na mwanawe wamerejea nchini na wako tayari kujibu mashataka.
Bi Wanjira, mumewe James Njenga Mungai na mwanao Antony wameshtakiwa kuizia kampuni ya stima ya KPLC mitambo ya transfoma feki.
Watatu hao ambao ni wakurugenzi wa kampuni ya Mulwa Trading Company wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kupokea pesa za umma kwa njia ya undanganyifu.
Bw Mungai alifikishwa kortini mnamo Julai 17 pamoja na waliokuwa wakuu wa kampuni ya Kenya Power Dkt Ben Chumo, Dkt Ben Tarus na mameneja wakuu wa KPLC.
Washtakiwa walikana mashataka ya kufanya njama za kuilaghai KPLC Dola za Kimarekani $4,081,920 (KSH408,192,000).
Watatu hao walishtakiwa kupokea kwa njia ya undanganyifu Dola za kimarekani ($)2,01`4,880 (Sh201,488,000) ikiwa ni mauzo ya transfoma feki.
Walidaiwa walipokea pesa hizo kati ya Agosti 2012 na Juni, 12 2018.
Bw Wandugi aliomba Wanjira na Antony waachiliwe kwa dhamana akisema “ ilibidi warudi nchini kujibu mashtaka kutoka Uingereza walipokuwa wakipokea matibabu.
“Naomba hii mahakama imkubalie Wanjira kuwa akirudi kupokea matibabu kila wakati Uingereza kwa vile anaugua ugonjwa unaohitaji kuonekana mara kwa mara na Daktari,” alisema Bw Wandugi.
Aliomba mahakama iwe ikimpa cheti chake cha kusafira kila wakati anapohitaji kusafiri.
Hakimu mkuu mahakama ya kuamua kesi za ufisadi Bw Douglas Ogoti alikubalia ombi la Bi Wanjira la kusafiri anapohitaji kuhudhuria matibabu.
Pia aliwaachilia kwa dhamana ya Sh1milioni pesa tasilimu.
Kiongozi wa mashtaka aliamriwa awape nakala za mashahidi