• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 8:50 AM
Wakurugenzi waliopunja Kenya Power Sh14.4m kutiwa nguvuni

Wakurugenzi waliopunja Kenya Power Sh14.4m kutiwa nguvuni

Na RICHARD MUNGUTI

WASHUKIWA 11 wa kampuni zilizouzia kampuni ya stima ya Kenya Power bidhaa Jumatano waliagizwa watiwe nguvuni kwa kukataa kufika kortini kujibu mashtaka ya ufujaji wa zaidi ya Sh14.4 milioni.

Hakimu mwandamizi Bw Lawrence Mugambi alifahamishwa baadhi ya wakurugenzi hao wa Millous Enterprises Limited, Kazimix Enterprises Limited, Petus Investiments Limited, Touchline Electrical Limited , Mint Ventures Ltd, Jake Building Construction , Apenco Holding Limited na Wachema hawakufika kortini kujibu mashtaka kama walivyokuwa wameamriwa.

Mahakama iliamuru watiwe nguvuni na kufikishwa kortini wakati wowote.

Washtakiwa hao waliamriwa wafike kortini jana kujibu mashtaka ya kupokea pesa kwa njia ya undanganyifu.

Bw Mugambi alielezwa kuwa washtakiwa hao 11 walikuwa wamepelekewa samanzi wafike kortini jana lakini wakakaidi.

“Washtakiwa walikuwa wameamriwa wajisalamishe kortini kujibu mashtaka lakini waliona heri wasifike,” alisema kiongozi wa mashtaka.

Mbali na kufika kortini washukiwa hao walikuwa wametakiwa wafike katika afisi ya mkurugenzi wa jinai (DCI) kuandikisha taarifa lakini hawakuenda.

Mahakama iliambiwa tabia hiyo ya kutoheshimu maagizo ya mahakama haipasi kustahimiliwa.

Korti iliombwa iamuru washikwe na kufikishwa kortini.

Kampuni ya Touchline pamoja na wakurugenzi wake Hillary Njaramba na Esther Nyambura wanakabiliwa na shtaka la kupokea pesa za umma Sh8,333,933 wakidai walikuwa wameteuliwa kutoa huduma za uchukuzi na ajira ya kibarua.

Shtaka lilisema walitekeleza uhalifu huo kati ya Aprili 12 2017 na June 12 2018.

Bw Mugambi aliombwa atenge Agosti 20 siku ya kutajwa kwa kesi hiyo ndipo upande wa mashtaka upewe fursa ya kuwatia nguvuni washtakiwa.

Mahakama iliamuru upande wa mashtaka utayarishe ushahidi kwa vile kesi ikianza haitasitishwa.

“Kesi hii ikianza kusikizwa haitaahirishwa,” aliamuru Bw Mugambi akiongeza , “Mradi kuwe na mtu mgonjwa mahututi.”

Mahakama iliombwa itoe kibali cha kuwatia nguvuni kwa vile , “washukiwa hao wameidharau mahakama na kamwe hawawezi kusamehewa kwa vile walijua wanatakiwa kufika kortini kujibu mashtaka nane dhidi yao.”

You can share this post!

Mama aliyemlaghai mwenzake mamilioni motoni

Polisi waliomuua mwanamke City Park nje kwa dhamana

adminleo