• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 9:12 AM
SGR kutoka Naivasha hadi Kisumu kugharimu Wakenya Sh380 bilioni

SGR kutoka Naivasha hadi Kisumu kugharimu Wakenya Sh380 bilioni

Na CHARLES WASONGA

UJENZI wa reli ya kutoka Naivasha hadi Kisumu utagharimu Sh380 bilioni, Sh53 bilioni zaidi ya gharama ya awamu ya kwanza ya reli hiyo kutoka Mombasa hadi Nairobi iliyogharimu Sh327 bilioni.

Katika ujumbe kupitia mtandao wa Twitter, katika wa idara ya Ubunifu, Dijitali na Mawasiliano ya Nje, Denis Itumbi Ijumaa alisema Waziri wa Uchukuzi James Macharia ataongoza ujumbe wa maafisa wa wizara yake kwenda China kusaka ufadhili kwa mradi huo.

Kukamilishwa kwa awamu hiyo ya tatu ya mradi wa SGR wa umbali wa kilomita 255 kutafikisha Sh887 bilioni gharama ya mradi huo mkuu katika utawala wa Rais Uhuru Kenyatta.

Reli hiyo ya awamu ya 2B, itapitia katika kaunti nne ambazo ni; Narok, Bomet, Kericho na Kisumu.

Kufikia sasa Sh327 bilioni zimetumika katika awamu ya kwanza ya mradi huo kutoka Mombasa hadi Nairobi kando na Sh150 bilioni zilizotumika kufadhili ujenzi wa awamu ya pili kutoka Nairobi hadi Naivasha.

Sasa kuna huduma ya treni kwa jina Madaraka Express ya uchukuzi wa abiri na mizigo kati ya Nairobi na Mombasa.

You can share this post!

Agosti 21 yatangazwa sikukuu ya Idd-ul-Azha

Niko tayari kuelewana na Ruto – Raila

adminleo