Habari Mseto

Ageuza shule yake chumba cha kuku

August 10th, 2020 1 min read

GEORGE MUNENE na FAUSTINE NGILA

Wakati serikali iliangiza kufungwa kwa shule kufuatia kuzuka kwa virusi vya corona, wamiliki wa shule za kibinafsi walipatikana hawajajiandaa.

Kwa kawaida shule hizo hupata mapato kwa karo inayolipwa na wazazi na kufungwa kwa shule kuliwatia wamiliki wa shule hizo kwenye matatizo ya kifedha.

Ili kukidhi mahitaji wengine wanatumia madarsa kufungia kuku.

Bw Joseph Maina ni mmmoja wa wamiliki wa shule za kibinafsi ambaye amebadilisha shule yake kuwa shamba la kufugia kuku.

Tayari Bw Maina anafunga kuku 1,100 ilialipe deni ya mkopo aliochukua ili kupanua shule yake ya Mwea Brethen kwenye mji wa Ngurubani kaunti ya Kirinyanga.

Anaazimia kufunga kuku 5,000 kufikia mwezi wa Desemba.

Bw Maina na bibi yake Beatrice kwa sasa wanafubga kuku ili kupata pesa za matumizi ,kulipa deni nan a kukidhi mahitaji ya watoto wao na kulipa madeni.

Wakati serikali ilisema shule zifungwe ,Bw Maina alifikiri kwamba matatizo ya corona hayatakua mengi ,lakini wakati shule zilikosa kufunguliwa baada ya miezi miwili Bw Maina alihisi hatari.