Dondoo

Demu aona siku ndefu baada ya kuweka picha ya mpenzi wake mpya Facebook bila idhini

Na JOHN MUSYOKI November 13th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

JAMAA wa hapa alimfokea kipusa mmoja mbele ya watu kwa kuweka picha zake kwenye mtandao wa ‘Facebook’ bila ruhusa yake.

Kimwana huyo alichukua hatua hiyo siku chache baada ya kuanzisha uhusiano na kalameni huyo.

Inasemekana demu alijawa na furaha tele kumwingiza jamaa boksi na akataka kumtambulisha kwa wenzake.

Hata hivyo, jamaa alipogundua kisura alikuwa akijigamba na kuanika picha zake mtandaoni kiholela, aliamua kumzomea kabla ya kukatiza uhusiano wao.

“Uliweka picha zangu mtandaoni bila ruhusa yangu. Nani alikwambia nimeamua kukuoa? Wacha kiherehere chako wewe!” jamaa alifoka.

Huo ndio uliokuwa mwisho wa uhusiano wa wawili hao. Kidosho alisalia akisaga meno na kujuta kwa kuanika mpenziwe mitandaoni bila idhini yake.