Donge nono la mpenzi bwanyenye lavuruga uhusiano wa dada wawili
NYALI, MOMBASA
KIPUSA wa hapa alimchemkia dadake kwa hasira akimlaumu kwa wivu alipopata mpenzi mwenye donge.
Kidosho huyo aliingizwa boksi na mwana wa bwanyenye mmoja eneo la pwani na dadake akaanza kuingiwa na wivu hasa baada ya jamaa kufika kwa wazazi na kupatiwa baraka za kuoa kipusa.
Juzi, alimsuta kidosho naye akashindwa kuvumilia na kumrushia cheche akitaka amkome.
“Uhusiano wetu ulikuwa sawa hadi nilipoanza mipango ya harusi ukaanza kunichukia.”
“Badala ya kuniombea mema unaanza kuvuruga mipango yangu na unafikiri sijui. Itabidi ukome kwa kuwa harusi itafanyika upende usipende,” kipusa alimfokea dadake.
Habari zilipofikia wazazi wao, wawili hao walipatanishwa ili wasiaibishe familia.