Mganga ajenga kanisa baada ya kuandamwa na msururu wa mikosi
MGANGA mmoja alishtua watu alipofungua kanisa na kugeuka mchungaji baada ya nyumba aliyokuwa akifanyia kazi kuchomeka mara kadhaa na vyombo vyake vya uganga kuharibiwa.
Nyumba ya kazi ya babu huyo ilichomeka mapema mwaka huu kwa mara ya kwanza, lakini moto huo ulizimwa upesi. Miezi miwili baadaye, nyumba hiyo hiyo ilishika moto tena ambao wakazi walimsaidia kuuzima.
Wiki hii, nyumba hiyo inayohifadhi nyenzo za kazi yake ilishika moto na kuchomeka yote na hakuna chochote kilichookolewa na jamaa akaamua kuokoka.Aliita mafundi na papo hapo shughuli za kujenga kanisa zikaanza.
Kwa sasa,kanisa hilo limekamilika huku likitarajiwa kufunguliwa hivi karibuni. “Ni kama Mungu anataka niachane na uganga nimgeukie,” jamaa alisema.