Mwanadada weita aliyetilia wateja ‘mchele’ kwa vinywaji atimuliwa kazini
MWANADADA aliyekuwa akihudumu katika baa ya hapa alipigwa kalamu teketeke kufuatia madai
kwamba amekuwa akiwatilia wanaume ‘mchele’ katika vinywaji vyao.
Meneja wa baa alisema kwamba alichukua hatua hiyo kufuatia malalamishi mengi kuhusu demu huyo.
Inadaiwa kidosho alikuwa akitilia wateja chembechembe za dawa hiyo ya kufanya mtu zuzu katika
vinywaji vyao kabla kuwapora hela.
Wateja walioathiriwa waliamua kuripoti kwa usimamizi kuhusu visa hivyo ili uchunguzi ufanywe.
Baada ya uchunguzi, meneja wa baa aliamuru kidosho huyo aondoke mara moja akidai amewaletea sifa mbaya na kufanya wateja wahamie kwingine.
Demu aliinuliwa juujuu na kufurushwa kama mbwa.