• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Akothee sasa aokoka, akimbia ‘tabu za dunia’

Akothee sasa aokoka, akimbia ‘tabu za dunia’

Na THOMAS MATIKO

MWANAMUZIKI mtatanishi na mjasiriamali Akoth Okeyo hivi majuzi alitangaza kuwa ameamua kuhamia kwenye muziki wa injili.? Siku chache zilizopita, alipohudhuria uzinduzi upya wa lebo ya msanii wa injili Kevin Bahati, EMB Records, Akothee alitapika nyongo.

?Mbona umeamua kuokoka??

Akothee: Mwanzo kabisa sijui kama kunaye mtu asiyemhitaji Yesu Kristo katika maisha yake. Kingine, muziki wa kidunia umejaa machungu.

Huna uhakika unayezungumza naye kama ni rafiki au adui. Wadau waliojaa ni wauaji vipaji. Hujui kama unayemwona kuwa wa karibu kwako kwenye gemu anakutakia mazuri au mabaya, hivyo hata kusukuma kazi zako inakuwa taabu.

Ila kwenye injili mambo ni tofauti kidogo. Kule mwanzo kanisa limejaa hata huhitaji kujisukuma sana hivyo nafikiri itakuwa rahisi kidogo kwangu.

Umetokea kuonyesha sapoti kwenye uzinduzi upya wa EMB Records,unaweza nawe ukawa na ndoto hizo??

Akothee: Kamwe haiwezekani kabisa.

Kwa sababu gani, wasanii wengi Kenya hawana heshima kabisa, ni wafitini, sio watu wa shukrani wamejaa machungu. Utamsaidia mtu kisha atakugeuka akupindishie maneno. Wanaturudisha nyuma.

Hivi hiyo ndiyo inaweza kuwa sababu ya wewe kufanya kolabo chache na wasanii wengi wa nyumbani??Akothee: Wapo wengi ambao wameniitisha kolabo.

Lakini unapompa utaratibu fulani, kesho unaamka kusikia stori tofauti mara atadai ninamtongoza nataka nitoke naye na vitu vingi vya kipuzi.

Watu hawajui tu mwenyewe nilivyohangaika kupata kolabo za kimataifa. Wakati mwingine hata nao hawaisapoti kazi ambazo umefanya nao. Hii tasnia yetu haijatulia ndio maana nimehamia ile ng’ambo ya pili.

Bila shaka wewe ni mjasiriamali wa kupigiwa mfano, lakini pia umeweza kumudu kwenye muziki kwa muda mrefu.

Umejifunza nini??

Akothee: Sote hatuwezi kuwa wanamuziki. Halafu ili kufanikiwa kwenye muziki lazima upambane.

Talanta pekee haitoshi. Asilimia 10% ni talanta na asilimia 90% iliyosalia ni kujituma na kutia bidiii. Ndio maana mimi nitawalazimishia hiyo kisiagi (staili ya muziki wake) mpaka muelewe na nafikiri tayari nishaeleweka. Lakini zaidi kabisa, nidhamu yako ndio itakayoamua mafanikio yako.

Hivi karibuni ulizua utata kwa staili yako ya mavazi, wengi wakikukashifu hasa kwa kuwa wewe ni mama??

Akothee: Hilo nalifahamu kabisa.

Na ndio maana ninachosema, ninachokifanya ni kwa ajili ya watoto wangu. Watu wasiumize akili, mimi sio kioo cha jamii ila ni kioo kwa wanangu. Ieleweke mimi ni mwanamke ninayejiheshimu, hata huko kwenye mavazi, navalia kwa kulingana na tukio.

Hebu niangalie leo nilivyovalia. Kwa nini sikuja kivingine. Watu huwa wepesi kuhukumu. Najielewa na najitambua sana na ndio sababu nimefanikiwa. Mengine sijali wa kusema na waseme watakavyo.

Pia ulitrendi sana baada ya kuchangisha mamilioni ya pesa kuwanunulia chakula wahanga wa njaaa kule Turkana, wapo waliodai ni kiki??

Akothee: Midomo tuliumbiwa nayo ya kazi gani. Lakini kikubwa zaidi ieleweke kuwa sikufanya vile ili kuichomea picha serikali hapana.

Nina historia kubwa na Turkana, kule ndiko nilikozaliwa na kulelewa wazazi wangu walipokuwa wakifanya kazi hivyo nina uhusiano wa dhati na Turkana na ndio sababu nilishindwa kuvumilia. Lazima ningefanya kitu, kwa wanaoniponda wao wamefanya nini.

Kwa asiyekuelewa akakuchukulia kuwa mtu unayependa drama utamweleza nini??

Akothee: Ndiyo, mwenzenu napenda drama ndio hulka yangu. Lakini katika hilo napenda nidhamu sababu mwenyewe najiheshimu. Mimi ni mjasiriamali tena bilionea, mwenye kisomo kizuri.

Mimi ni mama, tena pia ni staa na sijali kama wanipenda au kunichukia. Tayari mimi ni staa Afrika sasa ninacholenga ni kwenda kimataifa.

Kikubwa tena zaidi ni kwamba mimi ni kielelezo bora kwa wanangu tu. Kwa hiyo kila ninachokifanya ni kwa ajili yao, sio watu wengine na ndio sababu sijali ulimwengu unachosema.

[email protected]

You can share this post!

JAMVI: Atwoli amepiga jeki azma ya Joho kuingia Ikulu...

Je, Uhuru amefanikiwa kuzima ‘Tangatanga?

adminleo