Habari Mseto

Apewa dhamana ya Sh500,000 kwa kupokonya ajuza unga wa kilo mbili

November 7th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

 Na Titus Ominde

MAHAKAMA moja mjini Eldoret iliamuru mwanaume aliyeshtakiwa kutumia nguvu wakati wa kumyang’anya nyanya mmoja kilo mbili za unga wa mahindi awachiliwe huru kwa dhamana ya Sh500,000.

Mahakama iliambiwa kuwa Stephen Muthaita Kimani pamoja na watu wengine ambao hawakuwa kortini wakiwa wamejihami kwa visu na silaha nyingine butu, walimwibia Bi Mary Kamau kilo mbili za unga wa mahindi,runinga,simu ya mkono,mtungi wa gesi miongoni mwa bidhaa nyingine zenye thamani ya Sh36,900.

Wizi huo unadaiwa kutekelezwa katika mtaa wa Langas mjini Eldoret mnamo Oktoba 31. Kesi itasikizwa Novemba 14.

kuwa wakati wa kutekelezwa kwa wizi huo walitumia nguvu huku wakimtishia maisha mlalamishi iwapo angedhubutu kupiga mayowe.

Kimani alikana mashtaka dhidi yake mbele ya hakimu mkuu mwandamizi wa Eldoret Bw Harrison Barasa.

Hakimu aliamuru mshtakiwa kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 500,000 la sivyo azuiliwe katika gereza kuu la Eldoret hadi pale kesi hiyo itakaposikizwa mnamo Novemba 14.