Aponea kifo akivuka mto watu 20 wakifariki
Na STANLEY KIMUGE
Mwanafunzi wa chuo kikuu aliponea kifo akivuka mto wakati wa mvua nyingi na maporomoko ya ardhi eneo la Chesegon katika mpaka wa Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet yaliyoacha watu 20 wamefariki..
Bi Nancy Pyatich mwenye miaka 23 ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayesomea ualimu Chuo Kikuu cha Moi, aliruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali ya Moi, Eldoret alipokuwa amelazwa.
“Kulianza kunyesha saa kumi jioni hapo ndipo nilianza kusikia sauti zizizoeleweka kutoka mtoni. Nilikuwa kwa duka wakati wanaumme wawili walikuja wakikimbia wakisema kwamba mambo yangekuwa mabaya jioni hio kwa hivyo tutoroke.
“Tulianza kukusanya stakabathi za ndugu yangu na pesa kidogo,”alisema. Bi Pyatich alisema kwamba walianza kukimbia wakielekea Marakwe, hapo ndipo walingundua kwamba mto ulikuwa umevuja kingo zake na ukaanza kubeba nyumba.
“Sehemu hiyo inazungukwa na mito minne, tuliamua kukimbia kuelekea upande wa Pokot lakini mito huko ilikuwa imejaa, hapo ndipo tuliamua kupanda mti. Kwa bahati mbaya ndugu yangu hangeweza kukwea mti kwa haraka hapo ndipo nilibebwa na maji.”