• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Benki ya Co-op yazoa faida zaidi kutokana na riba

Benki ya Co-op yazoa faida zaidi kutokana na riba

Na BERNARDINE MUTANU

Benki ya Co-operative imetangaza ongezeko la asilimia 7.57 ya faida yake katika miezi sita ya mwanzo 2018.

Kukua kwa faida kulitokana na ongezeko la mapato yanayotokana na riba. Benki hiyo Alhamisi ilitangaza faida ya Sh7.14 bilioni katika kipindi hicho ikilinganishwa na Sh6.63 bilioni 2017.

Mapato kutokana na riba yalikua kwa asilimia 7.9 kutoka Sh19.25 bilioni hadi Sh20.8 bilioni katika kipindi hicho.

Mapato ya riba yaliongezeka kutokana na hatua ya benki hiyo kukopesha serikali ambapo mikopo kwa serikali ilipanda kwa asilimia 17.45 hadi Sh4.54 bilioni.

Uwekezaji katika hati za serikali ulipanda kwa asilimia 13(Sh9.7 bilioni, hadi Sh80.2 bilioni katika kipindi hicho kutoka Sh70.5 bilioni katika kipindi hicho 2017.

Mikopo kwa watu binafsu iliongezeka kwa asilimia 5.69 kutoka Sh15.26 bilioni hadi Sh16.13 bilioni.

You can share this post!

Mahindi ya Uganda yashusha bei ya unga hadi Sh86

Ripoti yaonyesha wabunge walitumia Sh25 milioni...

adminleo